TANZIA Mwenge Kijijini ina majonzi makubwa, wawili wafa ndani ya saa 24

TANZIA Mwenge Kijijini ina majonzi makubwa, wawili wafa ndani ya saa 24

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Hiki ni kisa cha kuhuzunisha, Mwenge Kijijini jijini Dar inalia, misiba ya watu wawili marafiki John Simba na Patrick a.k.a Masu a.k.a Masumbuko marafiki chanda na Pete.

Issue iko hivi, washikaji wote wawili walikuwa wakiumwa, John Simba alikuwa mgonjwa zaidi, na Masu alikuwa akiumwa pia ila fresh fresh kimtindo, akilala siku mbili, siku ya tatu mko naye mtaani mnakula mamboz.

Sasa juzi, Masu kakata moto, majonzi yametanda na mshikaji wake john Simba hana taarifa kwamba nigga wake kakata moto.

Jana sasa ,wakuda wamemjulisha kwamba mshikaji wako Masu kavuta. Duh mshikaji kapatwa na mshituko, akang'ata shuka.

Basi hii misiba yote ni Mwenge mitaa ya Bamaga hapa jirani kwa P Funk
 
Msibani kwa John Simba, ubavuni kwa Kebbys Hotel, Mwenge Kijijini Dar es Salaam
20230405_165823.jpg
 
Poleni sana wana wa Mwenge Kijijini kwa msiba ,nakumbuka kipindi hicho nikienda Ibadani Mwenge RC,nikipita kwa akina Kazimbaya

Baadae nikawa namuona John Simba akipiga debe hapo Bamaga,akijaza Hiace za Mwenge -Manzese,(miaka ya nyuma kidogo jamani)..tangulia mwamba John Simba..mbele yetu ,nyuma yako
 
Huyu John Simba alisoma na kaka zangu Mwenge Primary, nadhani ni miaka kati ya 45-48
inabidi nitazame vzr maisha yangu umri ushasogea.
kuna vitu lazima tukubali vipite ili tuishi muda mrefu kwa sasa haina ubishi tena lazima tujue tunachofanya na pia tunachokula ili angalau tujenge heshima katika uzee wetu.
 
Poleni sana wana wa Mwenge Kijijini kwa msiba ,nakumbuka kipindi hicho nikienda Ibadani Mwenge RC,nikipita kwa akina Kazimbaya

Baadae nikawa namuona John Simba akipiga debe hapo Bamaga,akijaza Hiace za Mwenge -Manzese,(miaka ya nyuma kidogo jamani)..tangulia mwamba John Simba..mbele yetu ,nyuma yako
Mwenyezi Awarehemu Wana. Nasi tuko njiani. Atujalie Mwisho Mwema.

Mwenge Kijijini inanikumbusha Mwalimu Chilumba na Mwalimu Zayumba. Miaka imekwenda Aisee!
 
Back
Top Bottom