Mwenge: Ni Mwanga Tu Au Kuna Uvumba Fulani Unafukizwa Ili Kupumbaza Watanzania? Is it Justified?.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,804
Reaction score
134,593
Wanabodi,

Hili ni swali tuu najiuliza kuhusu hizi mbio za Mwenge wa Uhuru zinazoendelea sasa. Kwenye Mwenge kinachokimbizwa nchi nzima, jee kweli ni ule mwanga tuu ili kumulikia na kuangazia, au ni ule moshi mzito mweusi kana kwamba kuna dawa fulani za uvumba zinazonyunyuziwa kama ubani, kisha zinatumika na Mwenge kuwafukiza Watanzania ili kuendelea kuwapumbaza ili waendelee....(naomba nisimalizie).

Rais Magufuli alipoingia tuu madarakani na kufuta maadhimisho ya sherehe muhimu kama ya Uhuru kwa hoja kuwa hazi justify the cost for spending so much kwenye sherehe tuu huku hospitali zetu zikikosa madawa na wagonjwa wanalala chini kwa ukosefu wa fedha. Moja kwa moja nilidhania kuwa sasa huu ndio utakuwa mwisho wa kuzungusha kwa Mwenge wa Uhuru. Lakini hali haikuwa hivyo.
Ingekuwa ni Amri Yake, Magufuli Angefutilia Mbali Mbio za Mwenge!, Jee Ni Amri ya Nani?!.

Hivyo hili ni swali kwa wenye ufahamu wa ndani kuhusu huu Mwenge, tuelezane ukweli jamani. Kinachozungushwa ni Mwenge lakini the essence ni ule mwanga tuu wa kumulikia au ni ule moshi unaofukizwa kama vile umetiwa mavumba fulani kuwapumbaza Watanzania?!.
. Kama Tanzania tunataka maendeleo ya kweli ni lazima tuwe very serious kwa kuachana na kuendekeza matukio stereotype na kumaitains positions ambazo ni redundancies just to maintain a status quo, kwa vile zilikuwepo! .

When are we gonna change? . Yaani kwa Magufuli huyu aliyefuta sherehe za Uhuru lakini ana maintain mbio za Mwenge, huu Mwenge una nini haswa? . Tuelimishane jamani!.
Jumatano njema.
Paskali
update.
Forojo Ganze (Master), mchawi maarufu aliyeanzisha Mwenge wa Uhuru
 
Kaka Pascal mimi nakumbuka ulikesha kijijini kwetu Ngonga nilikuwa primary darasa la tano,kutokana na kuwa na ufahamu kidogo kila kona nilikuwa naona watu wamelaliana sasa nikawa sielewi. Kesho shuleni tukaambiwa tuandike insha kuhusu mwenge kutokana na utoto nilichoandika acha walimu wacheke mpaka machozi yaliwatoka,mwenge haufai.
 
Mwenye akili angekuja na Idadi na thamani ya miradi iliyofunguliwa na Mwenge toka tupate uhuru VS Gharama zilizotumiwa na Mwenge.

Hii ndio njia ya kisayansi ya kuujadili mwenge !!
Duh, yaani unaakili za ajabu Sana jingalao , unatetea kila kitu, ngoja nikuulize, kwa mfano hiyo miradi ingezinduliwa Tu na mwenyekiti Wa mtaa eneo husika ingeathiri vipi hiyo miradi katika utendaji/uzalishaji wake?

Vipi gharama za kukimbiza mwenge nchi nzima zingejenga viwanda vingapi? Inakuaje Sherehe za Uhuru Ni haramu ILA sherehe za Mwenge Ni halali? Ni sawa na kusema hulikitimoto ila mchuzi wake unakunywa!!!

Watanzania sio wajinga kiasi hicho.
 
Mwenye akili angekuja na Idadi na thamani ya miradi iliyofunguliwa na Mwenge toka tupate uhuru VS Gharama zilizotumiwa na Mwenge.

Hii ndio njia ya kisayansi ya kuujadili mwenge !!

Unataka kusema kuna uhusiano wa ujenzi wa miradi ya maendeleo na mwenge? Je hakuna njia nyingine nzuri na rahisi za kuzindua miradi ya maendeleo?

Je fedha za mwenge (makato ya lazima kwa watumishi wa umma, michango ya lazima na hiari, kodi za wananchi nk) kweli zinahalalisha zinaa, wizi, vifo, unyang'anyi na machafu mengine yanayotokea kwenye mikesha na misafara ya mwenge?

Unajua hizo mbio huambatana na vifo/ajali nyingi tu? Unajua kweli historia ya mwenge wewe? Ni viongozi wangapi wa mbio za mwenge waliokufa muda mfupi baada ya kilele cha mbio au waliopatikana na maswahibu?
 
Wakati tunatafakari hilo, tujiulize pia ile Fimbo ya Malkia na Mwenge wa Olympic ambavyo vyote hutembezwa sehemu mbalimbali Duniani na hapa kwetu vimeshafika mara kibao, je vina uvumba? Au malengo yake ni nini?

Mkuu je vilipofika hapa kwetu, kulifanyika ufuska kama ilivyoelezewa hufanyika wakati wa mbio za mwenge wa uhuru?
 
Paskali;
Mimi si mganga wa kienyeji wala sina uganga/uchawi lakini nataka kukuunga mkono katika matamshi ulo tamka kuwa huenda kuna uvumba flani huwekwa ndani yake kuwapumbaza watz.
Hicho kinachowafanya wakuu wasione hiyo gharama ya kulilinda "bati" hilo kwa mbwe mbwe zoote. Lipigiwe ngoma za kienyeji usiku kucha, watoto wasio na baba wazaliwe/watungwe mimba sio chini ya 100 kila siku usiku mahali flani. Serekali isione hiyo hasara na hatari kwa taifa. Nasema hawataki kutuambia ila kuna jambo nyuma ya pazia. Uasherati unaofanyikaga kila mwenge unapokesha sio siriiiii. Magonjwa yanayoachwa hapo kijijini si ya kawaida. Iweje serekali iyapuuze iuone mwenge kuzimika ni hasara kuliko madhara yanayoletelezwa nao??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…