Kaka yangu Paschal
umesahau kitu kimoja
sherehe za Uhuru mwaka 2016 zilifanyika kama kawaida na nadhani zitaendelea kufanyika
Sherehe za Muungano zimeendelea kufanyika na sherehe nyingine zinaendelea kufanyika.
Ilifutwa sherehe ya Uhuru ile moja tu mwaka 2015.
Lakini pili kuhusu ufuska naona umeongelea sana
ha ha ha ha mi naonaga ufuska hufanyika kila mahala watu wanapokusanyika, hata kwenye makongamano ya dini kuna ufuska.
Nilihudhuria East Africa Youth Festival mwaka 2014 Arusha
nilistaajabu sana vijana walivokuwa wanafanya ngono hadharani na kwenye hostel zikiwa pea hata mbiki kwa wakati mmoja wao...ama kweli nijiona mshamba wa dunia hii...infact nilishangaa kupitiliza na nilikereka vya kutosha.
Vijana walijiachiaaaa ....tena kulikuwa na mataifa matano tabia zao zilifanana.
Yaani wabongo waliwashobokea wageni, na wageni waliwashobokea wabongo.
Kuhitimisha hili ufuska unaofanyika kwenye mwenge wala sio kwasababu ya kufukizwa..ha ha ha...ni watu tu kwakuwa wapo pamoja na wanashereheka wanaona wamalize na ngono kabisaaaa.
Lakini 3
Mwenge ni alama ya taifa, unapopitishwa unaleta umoja, uzalendo kwa taifa, kuna karahaa fulani mtu unasikia ukiona Mwenge...watu hushangilia na kufurahi.
Lakini pia mwenge huhamasisha maendeleo....miradi humalizika haraka, barabara huchongwa na usafi hufanyika...nimeona Ubungo barabara zimefagiliwa leo..ha ha ha.
Anyway
najua hutakubali maana ulishakuwa na majibu yako...ukasema hutashangaa kuona watu wanatetea hili...sijui umeleta hapa tuunge mkono hoja tu.