Mwenge: Ni Mwanga Tu Au Kuna Uvumba Fulani Unafukizwa Ili Kupumbaza Watanzania? Is it Justified?.

Mwenge: Ni Mwanga Tu Au Kuna Uvumba Fulani Unafukizwa Ili Kupumbaza Watanzania? Is it Justified?.

Mwenge haujadiliki kisayansi kwa sababu misingi na dhima yake si ya kisayansi..

NB: Kuna wakati huwa unapelekwa nyuma ya jukwaa na kutamkwa "tumaneno maneno yasiyoeleweka"..

Mkuu Paskali; mwenge ni zaidi ya moto ule.. Ni zaidi ya mwanga..!
Everything is science !
 
Aisee yanayofanyika kwenye mikesha ya mbio za mwingi ni dhambi tupu. Mikesha ya mwenge inachangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa maambukizi ya ukimwi, mimba zisizotarajiwa na kujifunza ulevi. Siku mwenge ukiwepo sehemu usiku ukipita asubuhi utakuta kondomu zilizotumika na pakiti na chupa za pombe kali zimetapakaa kwenye vichochoro.
 
MWENGE ni miongoni mwa mazindiko ambayo nyerere na wale wazee wa Bagamoyo waliambiwa na mfalme wa hii dunia wawe wanafanya ili kuwapumbaza raia kwa lengo la kuendelea kuwaongoza,ndiomaana siku ile tunapata uhuru waliambiwa ni lazima upelekwe mlima kilimanjaro saa 6 usiku,miongoni mwa mazindiko mengine aliyoyafanya ni kukusanya michanga/udongo kutoka mikoa yoote ya tanganyika na kwenda kufanya zindiko mahali fulani(sitapataja),haya mazindiko yamekuwa yakifanywa mara kwa mara na viongozi wa CCM kwa lengo la kuiroga nchi ndiomaana akili za watanzania ni tofauti na wakenya,waganda,wacongo na baadhi ya majirani zetu,watanzania ni wavivu na waoga sana waku-react pale maswala muhimu yanapotokea mfano,wizi wa kura,mfumuko wa bei,kodi kandamizi,miundombinu mibovu,hali duni ya maisha,uonevu wa polisi,ubadhilifu wa viongozi wetu,katiba bora,tume huru ya uchaguzi! na mengine mengi,ndiomaana Kenya Uganda Congo DRC na kwingine mambo kama hayo yakitokea huwa hapakaliki sababu akili zao sio mgando kama zetu sisi bado ule uchawi wa kupenda Amani tunao!
Kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda haya mazindiko yanakwisha nguvu yake sababu watanzania wengi wamekuwa aware nayo so ile nguvu inashuka kiwango chake ila kwa mikoa ambayo bado yananguvu hata uwezo wa raia wa huko wa kufikiria ni mdogo sana hiyo mikoa nikama Dodoma,Tabora,Lindi,Mtwara,Kigoma na Singida na Pwani, mikoa ambayo nguvu ya haya mazindiko ya CCM imeanza kupotea kabisa ni kama MWANZA,ARUSHA,KILIMANJARO,DSM na MBEYA akili za rai wa hii mikoa ni tofauti na mikoa mingine.
Nyerere ndio alikuwa mchawi wa CCM akishirikiana na wazee wa bagamoyo na wazee wengine 12 sitawataja hapa,baada ya nyerere kufa uchawi wa CCM akakabidhiwa Mzindakaya,stiven wassira ,Kingunge Ngombalemwilu na Andy Chande (Marehemu sasa), hao woote umri wao umekwenda na baadhi yao wapo taabani kisiasa na kiafya pia na hata wengine kuhama chama.Viongozi wengi wa kidini hapa Tanzania wanajua kuhusu haya mazindiko wapo ambao hufunga na kuomba ili kuyavunja kimesaidia sana kupunguza makali ya haya mazindiko.
Vita ya Kagera,Mafuriko ya Lindi Mtwara ,ajali ya MV Bukoba,ajali ya treni reli ya kati DODOMA,maajali ya mabasi,ajali ya watoto arusha,na mengine mengi ni miongoni mwa sadaka au mazindiko au kafara ambazo wamekuwa wakitoa,ndiomaana tunapokuwa tunakaribia uchaguzi ajali nyingi kubwa kubwa huwa zinatokea SIO BURE!
kwa makosa waliyofanya MWINYI,MKAPA NA JK walitakiwa wakamatwe na kushitakiwa lakini hapa Tanzania tunawashangilia mara tuwaonapo majukwaani akili zetu zimefungwa "TUMEROGWA" nijukumu la viongozi wetu wa dini kuweka maombi kuendelea kuvunja haya maagano ya shetani na CCM.
 

Attachments

  • wazee wa bagamoyo.JPG
    wazee wa bagamoyo.JPG
    36.4 KB · Views: 117
Woote ni kasumba tu. Mbona hamjadili mwenge wa Olimpiki? Afanyacho mzungu ndio bora, cha mswazi ndio kupoteza muda, Pumbafuuuuu!!
 
Mwenye akili angekuja na Idadi na thamani ya miradi iliyofunguliwa na Mwenge toka tupate uhuru VS Gharama zilizotumiwa na Mwenge. Hii ndio njia ya kisayansi ya kuujadili mwenge !!

Na mawazo kwamba miradi haiwez kufunguliwa mpaka mbio za mwenge ni ya nan?? Na je, nchi zilizoendelea walitegemea mwenge kufungua miradi ili waendelee??
 
Sikuwahi kabla kushuhudia mwenge wa Uhuru hasa mkesha, mwaka huu nikasema nijisogeze nione kuna nini.

Tangu Siku ile najikuta nimeanza kuwa MTU wa hovyo hovyo tu.

Neno la Mungu linasema linasema, "Mkimbiani shetani naye atawakimbia"!
 
Kuna kitu siyo bure, lakini ni imani ya kipumbavu watu wenye akili zao kuendelea kuamini katika hiki kisicho wazi.
 
Mkuu pascal, uliwahi kujiuliza kwanini mwenge haupelekwaji Makanisani na Misikitini kuweka mawe ya msingi au kufungua majengo??
 
Ina maana unataka tuamini kuwa miradi hiyo iliyozinduliwa na mwenge toka uhuru ilijengwa kwa fedha zilizotokana na mapato ya michango ya mwenge ama kodi zetu!
Wakizindua miradi bila mwenge kama wanavyofanya wkt mwingine kuna nn kitapungua!
 
Mwenge ni moja ya uzuzu mkubwa ambao bado unaoendelea nchi hii huku ukigunikwa na uonevu na manyanyaso makubwa kwa wafanyakazi wa Serikali hasa Walimu.
 
Wanabodi,

Hili ni swali tuu ninajiuliza kuhusu hizi mbio za Mwenge wa Uhuru. Huu Mwenge kinachokimbizwa kweli ni ule mwanga tuu ili kuangazia, au kuna dawa fulani za uvumba zinazonyunyuziwa kama kuchoma ubani, kisha zinatumika na Mwenge kuwafukiza Watanzania ili kuendelea kuwapumbaza ili waendelee....(naomba nisimalizie).

Rais Magufuli alipoingia tuu madarakani na kufuta sherehe za Uhuru kwa hoja kuwa hazi justify the cost for spending so much kwenye sherehe huku hospitali zikikosa madawa na wagonjwa wanalala chini kwa ukosefu wa fedha. Moja kwa moja nilidhania kuwa sasa huu ndio utakuwa mwisho wa kuzungusha hiki kitu kinachoitwa Mwenge wa Uhuru. Lakini hali haikuwa hivyo.

Kwa wenye ufahamu wa ndani kuhusu huu Mwenge, tuelezane ukweli jamani, ni Mwenge tuu wa kumulikiwa au tunafukizwa ubani wa kuwapumbaza Watanzania ili...
Leo Mwenge umezungushwa wilaya yangu ya Kinondoni kupitia Barabara yangu ya Goba Rd. Askari wa kuzuia magari wametandazwa tangu mapema asubuhi. Askari hao hawana zile radio call za mawasiliano kujua msafara wa Mwenge umefika wapi, watu tumesimamishwa nusu saa nzima!.

Msafara ulipopita mimi nilihesabu magari ya serikali tuu yalifika 50!. Does this kweli justify the cost time and resources kuzungusha Mwenge kumulika mchana? , au tunazungushiwa ubani kwa jina la Mwenge?.

Nakumbuka nikiwa mwandishi wa habari kijana, nilipangiwa kuzunguka na Mwenge mkoa fulani, shughuli haswa ni pale mahali ambapo Mwenge unakesha usiku kucha, kinachofanyika katika shamrashara hizo, ni hakuna kulala, na kusema la ukweli, ujana ni maji ya moto, ilikuwa ni hakuna kulala, utu unaondoka kabisa unageuka unyama!. Kuna mambo mtu mzima mwenye akili zake alikuwa hawezi kuyafanya mahali pa wazi kwa kisingizio ni gizani!. Yaa ilikuwa ni ukigusa tuu unaitikiwa anajisongeza pembeni kwenye kigiza giza mnamalizana, name kila kona mnaonana watu wakimalizana!. Hiyo ndio shughuli kuu ya Mwenge wakati wa usiku enzi hizo, maana ile shughuli ya kuzindua miradi iliyokwisha kuwepo siku nyingi na tayari inafanya kazi, inakuwa imeishafanyika mchana.

Kufuatia shughuli hiyo kuu ya usiku ya shamra shamra za Mwenge ya hakuna kulala na ile hali ya ujana, nilitamani kila mbio za Mwenge nipangiwe mimi!. Sasa hivi nimekuwa mtu mzima nikielekea uzeeni, sasa ndio najiuliza na kutafakari hivi niliwezaje kuyafanya yale niliyoyafanya kwenye mbio za Mwenge, au tena mahali pa wazi na makundi ya watu kila mtu akiyafanya hayo hayo na wake?. Halafu ukimaliza na huyu sio ndio umetosheka, akitokea na mwingine unakwenda tena, kule mnaoishana na yule aliyeanza naye akiwa na mtu mwingine!. Sasa ndio najiuliza ilikuwaje au kwenye ule moshi wa Mwenge kuna mavumba yananyunyuziwa ili kufukizwa ukinusa tuu unapumbazika na kuweza kufanya lolote popote? .

Kama ni pombe mbona kila siku tunakunywa na ukitokea uhitaji utatafuta guest ya karibu kujipumzisha lakini kwenye mbio za Mwenge ni kutafuta kona ya giza na makundi ya watu bila aibu yoyote, yaani binadamu tunakuwa kama wanyama!.

Kuna wanaodai mahali Mwenge unapolala huchaguliwa kwa makini, na kudai kuwa mahali hapo hufanyika matambiko fulani ya kimila, na kutolewa kafara!, japo mimi nimeshiriki kuripoti mbio za Mwenge na kulala unapolala, sikuwahi kuona matambiko yoyote, wala kafara zozote zikitolewa, au kwa sababu likiisha ingia giza, mimi mawazo yangu yanahamia kwenye burudani za shamrashamra za usiku, na kuwa bize na yale mengine hadi kutoona matambiko wala kafara!. Wenye ushahidi na hili zaidi ya huyu, Siri ya Mwenge wa Uhuru
jitokezeni.

Kama tuliweza kusitisha very important event ya maadhimisho ya Uhuru, alafu uki determine the cost, the time and the resources allocated kwenye mbio za Mwenge, lazima ujiulize kweli Mwenge huu ni kumulika tuu au kuna kitu kingine muhimu nyuma yake?!.

Mafuta Ya Mwenge na Sumu ya Cabon.
Wakemia huu Mwenge unatumia mafuta gani yenye moshi mweusi mzito hivyo?. Kwa msio jua moshi mweusi ni sumu ya cabon ukivutwa sana husababisha magonjwa ya TB, Bronchitis na Cancer. Jee kuliwahi kufanyika utafiti hao wakimbiza Mwenge hua wanaishi muda gani humu duniani baada ya mbio za Mwenge?.

Kama lengo la Mwenge ni ule mwanga ili umulike, ulipoanzishwa ile 1961 hiyo ndio ilikuwa technology ya wakati huo, leo miaka 50 baadae kuna technology kibao za kuzalisha mwanga tena mkali zaidi ya huo wa mafuta yenye sumu, kwa nini tuendelee kuwauwa Watanzania wenzetu kwa sumu huku kuna lots of alternatives ambazo hazina sumu.

Hivi tungetumia source ya gesi badala ya mafuta ya Mwenge na tungesave kiasi gani?.

Badala ya kutumia hayo mafuta mazito yenye sumu kibao ya carbon, kwa nini tusingetumia methene ambayo ina mwanga na haitoi moshi?, au pia maelekezo ya mafuta hayo ya Mwenge pia ni maelekezo ya mganga wa Mwenge na hakuwahi kuulizwa kama tunaweza kuyabadili?.

Vijana wa UVCCM mliyemo humu, njooni na idadi ya wakimbiza Mwenge toka Uhuru, mtueleze wangapi wako hai hadi leo. Na kama kuna waliotangulia mbele ya haki ni wangapi, sababu za vifo vyao na kama ni maradhi ni maradhi gani na yaliwapata muda gani tangu baada ya mbio za Mwenge?.

Hata hivyo sitashanga kama watatokea watetezi wa kujustify this lavish spending and time wasting kama ilivyotokea mjadala wa umuhimu wa wakuu wa wilaya, ma DC ambao Katiba ya Warioba iliwafutilia mbali na kazi zao kufanywa na Wakurugenzi wa Halmashauri.

Kama Tanzania tunataka maendeleo ya kweli ni lazima tuwe very serious kwa kuachana na kuendekeza matukio stereotype na kumaitains positions ambazo ni redundancies just to maintain a status quo, kwa vile zilikuwepo! .

When are we gonna change? . Yaani kwa Magufuli huyu aliyefuta sherehe za Uhuru lakini ana maintain mbio za Mwenge, huu Mwenge una nini haswa? . Tuelimushane jamani!.
Jumatano njema.
Paskali

Mwenge pamoja na kwamba hauna faida wala manufaa yeyote kwa TAIFA zaidi ya kulea magonjwa tu,na sitashangaa kama 90% ya wakimbiza Mwenge wameshaondoka duniani au ni waathirika wa HIV.

Ukiangalia budget ya Mwenge unaweza kujenga dispensary zenye kiwango cha kati yaani kituo kinachoweza hata kulaza idadi kidogo ya watu na kuwa na mortuary.

Na bado unawachangisha walimu na wafanyakazi wa serikali ili wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wapate ulaji wao.

Inshort Mwenge ni chombo cha kupumbaza watanzania,ukitaka kuhakikisha ona UVCCM walivyo
 
Back
Top Bottom