Mafanikio kwenye haya mambo si kujua coding tu.
Kuna suala zima la networking, management, marketing, grit.Kupambana kuangalia mambo ya kodi imekaa vizuri wapi, governance, compliance, encryption for data at rest and in motion, PCI complince / retention, ransomware threats, breaches, talent iko wapi. Mwanzo mgumu.
Na hapo unaweza kumuonea Benjamin, kwa sababu ingawa inawezekana kasoma hizo shule na kupata networks fulani, ila na yeye kasota kufanyia kazi mafanikio anayopata. Na ana njaa ya kupata mafanikio zaidi. Naona team yake wanavyohangaika kuwa visible, kufanya outreach, kujimix na communities.
NALA nafikiri imekaa zaidi kwenye money transfers za kimataifa, na inashindana na makampuni makubwa ya kimataifa kama World Remit na Sendwave. Watanzania wa nje wana nafasi kubwa ya kuikubali na kuifanya ifanikiwe au kuipotezea tu.