6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,819
- 5,996
Niaje waungwana
Kwa kile kilichotokea jana hapo K'koo, mimi nashauri kwanza mwenye ghorofa lililoanguka akamatwe, mali zake zifilisiwe, na kiwanja kilichokuwa na jengo kiuzwe ili hela zitakazopatikana zitumike kuwasaidia wale wote waliojeruhiwa na waliofiwa na baba zao, wame zao, wake zao, watoto wao nk.
Ni ukweli ulio wazi kwamba baada ya msiba huu wa taifa kuisha na kila mtu kuendelea na maisha yake, kuna ndugu zetu ambapo watabakia na ulemavu wa kudumu, kuna watu ambao watabakia mayatima baada ya kupoteza baba au mama katika janga hilo. Sasa watu wa aina huyo ni nani atakaewasaidia kuwasomesha, kuwalea, kuwahudumia nk.
Najua kwa upande wa serikali ni vigumu sana wahanga kupata msaada hapo baadae. Maana janga likishaisha kila mtu ataelekea ya kwake, hivyo waliofiwa na wazazi wao hawatopata msaada tena. Kwa nchi za wenzetu ile bajeti inayotengwa kila mwaka kwa ajili ya majanga ingetumika kuwasaidia waliokumbana na majanga hayo japo kwa kuwapa mitaji waathirika.
Lakini kwa nchini kwetu ndo hivyo tena, fedha za majanga zinaishia kutumiwa na viongozi fulani kwa kununua viwanja na kujenga majengo makubwa makubwa huko Mbweni, Salasala, Bunju nk.
Halafu yanapotokea majanga ya ghafla kama haya unakuta wanakuja na majembe pamoja na kuleo kuchimbia kifusi kizito cha tani zaidi ya 50. Kuna watu wameachwa yatima wengine wamepoteza viungo vyao kizembe kwa sababu ya tamaa ya mtu mmoja.
Hivyo huyo mtu aadhibiwe kwa kunyang'anywa kiwanja ili kuizwe na hela kupelekwa kwa wahusika, hii ikiwa pamoja na kutaifisha mali zake zote alizochuma iwe kihalali au kiharamu ili kufidia hasara aliyowapa wenzake hapa duniani na pia iwe fundisho kwa wapumbavu wengine wenye mawazo finyu kama yake.
Soma Pia: Ghorofa limeporomoka Kariakoo asubuhi ya leo Novemba 16
Ushauri mzuri kwa mamlaka na wahusika mbali mbali.
RIP kwa watanzania wenzetu wote waliokufa katika ajali hiyo. Na wale waliopata majeraha Mungu muweza wa yote awaponye.
Asanteni