Mwenye jengo akamatwe, eneo liuzwe, mali zake zifilisiwe, halafu hela zote wapewe majeruhi na waliofiwa

Mwenye jengo akamatwe, eneo liuzwe, mali zake zifilisiwe, halafu hela zote wapewe majeruhi na waliofiwa

RIP kwa watanzania wenzetu wote waliokufa katika ajali hiyo. Na wale waliopata majeraha Mungu muweza wa yote awaponye.
Mmiliki ni yule Mchagga mtata sasa sijui unaanzia wapi maana ana kundi lake la madon wa town ambalo hata Serikali inawahanya
 
Mleta mada una mhemko sana, jaribu kujituliza ripoti ya uchunguzi ikitoka ukweli utabainika
Report huwa zinatoka nyingi zikiweko zile za moto sokoni kariakoo, karume, mwenge nk na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa.
 
Unajua sababu iliyosababisha jengo hilo kuanguka lakini au umekuja tu kumtetea mwenye jengo?

Angekuwa ni swala la moto ingeeleweka, lakini kulazimisha kuchimba chini ili ufosi kujenga underground sehemu isiyotakiwa kuchimbwa underground alaf unakuja kumtetea!
Yule Mchagga mtata unamjua lakini au ndio unajizima data?
 
Kariakoo wange-replan upya hilo eneo matathalani hilo lingebaki eneo la wauzaji wa nguo pekee, maeneo mengine yaanzishwe kuweka watu wa bulding materials, stationeries simu na vifaa vyake ili mwisho wa siku maeneo muhimu mfano ya assembly point na disaster rescue access point ziwepo.

serikali ianzishe maeneo mengine ambayo yata serve kama Kariakoo lkn kwa bidhaa ambazo pekee zitakuwa zinapatikana maeneo hayo, so hata population itapungua maana wahitaji watakuwa wanaenda eneo specific kwa ajili ya kufuata huduma/ bidhaa zinazopatikana mahali hapo, Shida ss Kariakoo inayotokea ni kwa sababu eneo limekuwa centralised kwa bidhaa zozote wenyewe wanasema karikaoo kila kitu kinapatikana...u
Kkoo iwe kwa maduka ya JUMLA TU...NA PIA STOO ZA SHEHENA ZITOKAZO BANDARINI...Masoko ya rejereja kila manispaa.....kisha masoko makubwa ya rejereja yawe Tmk, ilala, ubungo, kinondoni na kigamboni, kibaha, bagamoyo..ambayo feeder/Supplier mkubwa awe KKOO.
 
Labda vitengenezwe feki maana aliajiri fundi maiko abomoe kuta zinazoshika mjengo

Mtu ana gorofa na kodi zinaingia kila mwezi ameshindwa kuleta wataalamu na wajenzi wa maana ambao kwanza wangeweka nguzo kubwa kabda ya kubomoa hizo kuta
Sasa fundi maiko anasema tulivunja kutumia nyundo kumbe ndio kuta za nyumba walitaka ziwe za nini
Just imagine mkuu.. Bora hata ulivyomjibu huyo mtetezi wa matajiri uchwara.
 
Report huwa zinatoka nyingi zikiweko zile za moto sokoni kariakoo, karume, mwenge nk na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa.
Sasa ndio ukae kwa kutulia hizo issue za madon wa town ambao hata Serikali hutaona wakiwaongelea sana sana wataongea kwa upole
 
Yule Mchagga mtata unamjua lakini au ndio unajizima data?
Kutokumjua huyo mchaga ndo kinakataza watu tusitoe ushauri wa nini kifanyike ili kufidia hasara ya wale waliofiwa, filisika na kupata ulemavu wa kudumu kupitia hilo jengo mkuu.

Haya sasa wewe mwenye kumjua ungetuambia kwa kifupi au kirefu kumhusu huyo mchaga.
 
Serikali yako imemkalia kimya sababu inamjua ni mtata na hayupo mwenyewe ana genge lake behind ndio maana husikii hata mmoja anaemnyooshea kidole
 
TUNGEWEZA KUTUKMIA NJIA YA ASILI,

TUNGEPANGA MISTARI KUMI,
WENGINE WANAJAZA UDONGO KWENYE NDOO.

WENGINE KWENYE FOLENI TUNAJAZA MALOLI 200 MENDE.

NDANI YA MASAA KUMI KUSINGEKUWA NA KIFUSI WATU WOTE WANGEPONA.

SELIKALI HAINUNUI HATA MITAMBO YA UOKOAJI.

NI LAANA KWA MTU MWENYE AKILI TIMAMU KUZALIWA KWENYE HILI TAIFA
 
Inasikitisha sana na kufikirisha
Watu tumepoteza watanzania wenzetu kwa sababu ya tamaa ya mpumbavu mmoja. Halaf anakuja mtu hapa JF kumtetea muuaji. Inashangaza na kusikitisha sana.
 
Elimu mkuu utakuta hana elimu kabisa halafu watu wanabeza elimu
Mjinga kama huyo sasa ime cost gorofa lote kuporomoka na kupoteza maisha na pia mali za watu ambazo sidhani kama watazipata tena
Kweli ndio yale ya Musukuma kutukana wenye elimu
Hao matajiri wengi hawana elimu hata ya kuvukia barabarani
Matajiri huko ni uchwara tu

Ova
 
Niaje waungwana

Kwa kile kilichotokea jana hapo K'koo, mimi nashauri kwanza mwenye ghorofa lililoanguka akamatwe, mali zake zifilisiwe, na kiwanja kilichokuwa na jengo kiuzwe ili hela zitakazopatikana zitumike kuwasaidia wale wote waliojeruhiwa na waliofiwa na baba zao, wame zao, wake zao, watoto wao nk.

Ni ukweli ulio wazi kwamba baada ya msiba huu wa taifa kuisha na kila mtu kuendelea na maisha yake, kuna ndugu zetu ambapo watabakia na ulemavu wa kudumu, kuna watu ambao watabakia mayatima baada ya kupoteza baba au mama katika janga hilo. Sasa watu wa aina huyo ni nani atakaewasaidia kuwasomesha, kuwalea, kuwahudumia nk.

Najua kwa upande wa serikali ni vigumu sana wahanga kupata msaada hapo baadae. Maana janga likishaisha kila mtu ataelekea ya kwake, hivyo waliofiwa na wazazi wao hawatopata msaada tena. Kwa nchi za wenzetu ile bajeti inayotengwa kila mwaka kwa ajili ya majanga ingetumika kuwasaidia waliokumbana na majanga hayo japo kwa kuwapa mitaji waathirika.

Lakini kwa nchini kwetu ndo hivyo tena, fedha za majanga zinaishia kutumiwa na viongozi fulani kwa kununua viwanja na kujenga majengo makubwa makubwa huko Mbweni, Salasala, Bunju nk.

Halafu yanapotokea majanga ya ghafla kama haya unakuta wanakuja na majembe pamoja na kuleo kuchimbia kifusi kizito cha tani zaidi ya 50. Kuna watu wameachwa yatima wengine wamepoteza viungo vyao kizembe kwa sababu ya tamaa ya mtu mmoja.

Hivyo huyo mtu aadhibiwe kwa kunyang'anywa kiwanja ili kuizwe na hela kupelekwa kwa wahusika, hii ikiwa pamoja na kutaifisha mali zake zote alizochuma iwe kihalali au kiharamu ili kufidia hasara aliyowapa wenzake hapa duniani na pia iwe fundisho kwa wapumbavu wengine wenye mawazo finyu kama yake.

Soma Pia: Ghorofa limeporomoka Kariakoo asubuhi ya leo Novemba 16

Ushauri mzuri kwa mamlaka na wahusika mbali mbali.

RIP kwa watanzania wenzetu wote waliokufa katika ajali hiyo. Na wale waliopata majeraha Mungu muweza wa yote awaponye.

Asanteni
Halafu wewe ndio unakuja kupewa uongozi au hata ukuu wa mkoa nahisi utachinja sana watu,uongozi ni hekima na busara
 
Kuna wakati nlikuwa karibu sana na jamaa mmoja alikuwa na asili ya kiarabu smbdy kanji...kuna kazi zake fulani alikuwa ananipaga namfanyia
Alikuwa na yard ya magari alihassan mwinyi Road upande ule wa kuelekea best bite
Kwenye mazungumzo alikuwa anasema nataka kushusha ghorofa hapa ila nataka nije npate nyumba kama 5...yule mwamba alikuwa na mkakati na pesa ilikuwepooo sema alikuwa low profile
Alikuwa na usemi wake anasema mm nkikupa offer ukikataa basi hutakuja ipata popote
Aliwahamisha watu pLe na wengine mpk nyumba aliwanunulia....akaja kqwli kushusha kitu faykat tower jengo linampaka underground,ila alikuja kufariki ila watoto zake wanaendelea vzr tu
Ujenzi wake ulikuwa si wa kubahatisha
Sasa hawa wakinga na wengine huko kko wanajenga magorofa kihuni uchafu tu

Ova
Mtu anaokota mafundi mitaan, anawalipa hela kidogo ili wamjengee mjengo mkubwa. Na wao ili kufidia ile hela ndogo waliyopewa wanaamua kuchanga cement kidogo na iliyobakia wanaiba.

Mwisho wa siku baada ya ghorofa kuisha au kabla ya kuisha, ndo yanatokea majanga kama haya yaliotokea K'koo.
 
Watu tumepoteza watanzania wenzetu kwa sababu ya tamaa ya mpumbavu mmoja. Halaf anakuja mtu hapa JF kumtetea muuaji. Inashangaza na kusikitisha sana.
Wewe kafungue kesi ya kumfirisi mwenye Jengo maana unaambiwa ni Umoja wewe umekaza kichwa, Serikali yako yenyewe haijamnyooshea kidole sio kwamba haimjui au haiwajui wenye Jengo
 
Kuna wakati nlikuwa karibu sana na jamaa mmoja alikuwa na asili ya kiarabu smbdy kanji...kuna kazi zake fulani alikuwa ananipaga namfanyia
Alikuwa na yard ya magari alihassan mwinyi Road upande ule wa kuelekea best bite
Kwenye mazungumzo alikuwa anasema nataka kushusha ghorofa hapa ila nataka nije npate nyumba kama 5...yule mwamba alikuwa na mkakati na pesa ilikuwepooo sema alikuwa low profile
Alikuwa na usemi wake anasema mm nkikupa offer ukikataa basi hutakuja ipata popote
Aliwahamisha watu pLe na wengine mpk nyumba aliwanunulia....akaja kqwli kushusha kitu faykat tower jengo linampaka underground,ila alikuja kufariki ila watoto zake wanaendelea vzr tu
Ujenzi wake ulikuwa si wa kubahatisha
Sasa hawa wakinga na wengine huko kko wanajenga magorofa kihuni uchafu tu

Ova
Hili naamini kabisa lipo kwani kuna mzee pia alijenga mjengo hapo na alitaka jengo liwe na sehemu ya kushushia mizigo yake chini kutokana na zahma za hapo sokoni
Ila alitoa hela nyingi sana kukamilisha zoezi mzee huyo anauza matairi ya jumla toka nje na kibunda anacho
Malori yanaenda underground kushusha mizigo bila usumbufu

Huyu mjinga kaona awalipe cheap labour wakashushe gorofa kwa masaa
 
Mtu anaokota mafundi mitaan, anawalipa hela kidogo ili wamjengee mjengo mkubwa. Na wao ili kufidia ile hela ndogo waliyopewa wanaamua kuchanga cement kidogo na iliyobakia wanaiba.

Mwisho wa siku baada ya ghorofa kuisha au kabla ya kuisha, ndo yanatokea majanga kama haya yaliotokea K'koo.
Zile NONDO duuh MAFUNDI maiko hawaendi mbinguni
 
Back
Top Bottom