Mwenye jengo akamatwe, eneo liuzwe, mali zake zifilisiwe, halafu hela zote wapewe majeruhi na waliofiwa

Mwenye jengo akamatwe, eneo liuzwe, mali zake zifilisiwe, halafu hela zote wapewe majeruhi na waliofiwa

Hadi sasa imeripotiwa idadi ya wenzetu wangapi waliotutangulia?
Mwanzo ilikuwa wa5, lakini kwa sasa idadi imeongezeka japo sijui wamefikia wangapi. Ni kuwaombea na kutafuta njia ya kuwaokoa waliobakia chini ya kifusi.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Kama ana vibali halali vya kumiliki na kufanya maboresho aliyokuwa anafanya kama ni kweli, basi hagusiki?
Labda vitengenezwe feki maana aliajiri fundi maiko abomoe kuta zinazoshika mjengo

Mtu ana gorofa na kodi zinaingia kila mwezi ameshindwa kuleta wataalamu na wajenzi wa maana ambao kwanza wangeweka nguzo kubwa kabda ya kubomoa hizo kuta
Sasa fundi maiko anasema tulivunja kutumia nyundo kumbe ndio kuta za nyumba walitaka ziwe za nini
 
Mwanzo ilikuwa wa5, lakini kwa sasa idadi imeongezeka japo sijui wamefikia wangapi. Ni kuwaombea na kutafuta njia ya kuwaokoa waliobakia chini ya kifusi.
Inahuzunisha sana
 
Jaribuuuu uoneerr 1bil hupati 20 x 20 ...

Wewe unasemajeeer
Ni kweli ila hiyo inatokana na udhaifu wa serikali.

Waziri husika wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi yupo zake ziarani huko mikoani. Ni kama vile haya yaliotokea yametokea nchi jirani sio Tz hivyo hayamuhusu.
 
Labda vitengenezwe feki maana aliajiri fundi maiko abomoe kuta zinazoshika mjengo

Mtu ana gorofa na kodi zinaingia kila mwezi ameshindwa kuleta wataalamu na wajenzi wa maana ambao kwanza wangeweka nguzo kubwa kabda ya kubomoa hizo kuta
Sasa fundi maiko anasema tulivunja kutumia nyundo kumbe ndio kuta za nyumba walitaka ziwe za nini
Matajiri wa kukinga na wachaga kko wazushi tu kuanzia ujenzi,mafundi wao ,material zenyewe nyingi ni za uwizi shotkut
Mpaka hapo suala vibali unafikiri litakuwaje

Ova
 
Ni kweli ila hiyo inatokana na udhaifu wa serikali.

Waziri husika wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi yupo zake ziarani huko mikoani. Ni kama vile haya yaliotokea yametokea nchi jirani sio Tz hivyo hayamuhusu.
Kkooni ya PM waxiri Fedha na Mama mwenyewe wengine pale huruhusiwi kusogeaaa.....kitovu cha uchumi wa SaDCC sio tu EAC....oohhj jomba stuka kaa mbaliii
 
Umewahi miliki ghorofa ? , au ndio wale mnaotaka matajiri waishi kama mashetani ?

Nadhani la msingi Serikali kusimamia ubora na viwango vya majengo kikamilifu pasipo kupepesa macho
 
Labda vitengenezwe feki maana aliajiri fundi maiko abomoe kuta zinazoshika mjengo

Mtu ana gorofa na kodi zinaingia kila mwezi ameshindwa kuleta wataalamu na wajenzi wa maana ambao kwanza wangeweka nguzo kubwa kabda ya kubomoa hizo kuta
Sasa fundi maiko anasema tulivunja kutumia nyundo kumbe ndio kuta za nyumba walitaka ziwe za nini
Matajiri wengi kko malofa tu
Wanapenda urahisi

Ova
 
Umewahi miliki ghorofa ? , au ndio wale mnaotaka matajiri waishi kama mashetani ?

Nadhani la msingi Serikali kusimamia ubora na viwango vya majengo kikamilifu pasipo kupepesa macho
Hakuna maghorofa huko kuna uchafu tu

Ova
 
Niaje waungwana

Kwa kile kilichotokea jana hapo K'koo, mimi nashauri kwanza mwenye ghorofa lililoanguka akamatwe, mali zake zifilisiwe, na kiwanja kilichokuwa na jengo kiuzwe ili hela zitakazopatikana zitumike kuwasaidia wale wote waliojeruhiwa na waliofiwa na baba zao, wame zao, wake zao, watoto wao nk.

Ni ukweli ulio wazi kwamba baada ya msiba huu wa taifa kuisha na kila mtu kuendelea na maisha yake, kuna ndugu zetu ambapo watabakia na ulemavu wa kudumu, kuna watu ambao watabakia mayatima baada ya kupoteza baba au mama katika janga hilo. Sasa watu wa aina huyo ni nani atakaewasaidia kuwasomesha, kuwalea, kuwahudumia nk.

Najua kwa upande wa serikali ni vigumu sana wahanga kupata msaada hapo baadae. Maana janga likishaisha kila mtu ataelekea ya kwake, hivyo waliofiwa na wazazi wao hawatopata msaada tena. Kwa nchi za wenzetu ile bajeti inayotengwa kila mwaka kwa ajili ya majanga ingetumika kuwasaidia waliokumbana na majanga hayo japo kwa kuwapa mitaji waathirika.

Lakini kwa nchini kwetu ndo hivyo tena, fedha za majanga zinaishia kutumiwa na viongozi fulani kwa kununua viwanja na kujenga majengo makubwa makubwa huko Mbweni, Salasala, Bunju nk.

Halafu yanapotokea majanga ya ghafla kama haya unakuta wanakuja na majembe pamoja na kuleo kuchimbia kifusi kizito cha tani zaidi ya 50. Kuna watu wameachwa yatima wengine wamepoteza viungo vyao kizembe kwa sababu ya tamaa ya mtu mmoja.

Hivyo huyo mtu aadhibiwe kwa kunyang'anywa kiwanja ili kuizwe na hela kupelekwa kwa wahusika, hii ikiwa pamoja na kutaifisha mali zake zote alizochuma iwe kihalali au kiharamu ili kufidia hasara aliyowapa wenzake hapa duniani na pia iwe fundisho kwa wapumbavu wengine wenye mawazo finyu kama yake.

Soma Pia: Ghorofa limeporomoka Kariakoo asubuhi ya leo Novemba 16

Ushauri mzuri kwa mamlaka na wahusika mbali mbali.

RIP kwa watanzania wenzetu wote waliokufa katika ajali hiyo. Na wale waliopata majeraha Mungu muweza wa yote awaponye.

Asanteni
Hakuna viongozi wa kufanya hayo kwa SASA hivi. Viongozi unaotegemea wachukue hatua hizo ndio haohao wanaokuwa wa Kwanza kunufaika na haya madhila
 
Umewahi miliki ghorofa ? , au ndio wale mnaotaka matajiri waishi kama mashetani ?

Nadhani la msingi Serikali kusimamia ubora na viwango vya majengo kikamilifu pasipo kupepesa macho
Unajua sababu iliyosababisha jengo hilo kuanguka lakini au umekuja tu kumtetea mwenye jengo?

Angekuwa ni swala la moto ingeeleweka, lakini kulazimisha kuchimba chini ili ufosi kujenga underground sehemu isiyotakiwa kuchimbwa underground alaf unakuja kumtetea!
 
Matajiri wengi kko malofa tu
Wanapenda urahisi

Ova
Elimu mkuu utakuta hana elimu kabisa halafu watu wanabeza elimu
Mjinga kama huyo sasa ime cost gorofa lote kuporomoka na kupoteza maisha na pia mali za watu ambazo sidhani kama watazipata tena
Kweli ndio yale ya Musukuma kutukana wenye elimu
Hao matajiri wengi hawana elimu hata ya kuvukia barabarani
 
Back
Top Bottom