Mwenye jengo akamatwe, eneo liuzwe, mali zake zifilisiwe, halafu hela zote wapewe majeruhi na waliofiwa


Akamatwe haraka Sana kwa kosa la Negligence
 

Kweli kabisa mkuu.
 
Anaweza kuwa na vibali halali vya umiliki wa eneo, lakini sidhani kama anaweza kuwa na vibali halali vya kuchimba underground. Huyo alitumia uhuni kwa kuwahonga watu wachache kwenye mamlaka ili wamuache ajenge tu atakavyo. Sasa imekula kwake.

Alifanya Jambo la hatari Sana. Na wote waliomruhusu inatakiwa wachukuliwe hatua.
 
Hivi ndio maskini wanavyotamani matajiri washuke wawe kama wao.


Tajiri sio injinia. What if alishauriwa kitaalam kwamba inawezekana?? Subirini uchunguzi ufanyike na mmiliki ahojiwe, acheni roho za kwanini, tatizo sio mmiliki peke yake, ujenzi mkubwa kama huo unahitaji approval na huenda mamlaka husika waliidhinisha.​
 
vip kuhusu ajali za barabani, majanga ya moto na ajali za boti majini, njaa, ukame , mafuriko n.k nani awajibishwe na kwa style ipi?🐒

Tofautisha man made calamitiea na force majeure calamities. Ajali ya kariakoo ni man made calamity sio force majeure Kama tetemeko au mafuriko. Uwe mtu mwelewa saa zingine.
 
Mkuu mwenye Jengo Hana shida.. Hapa WA kufilisi ni wale waliotia sahihi na mihuri kwenye vibali hawa wanapaswa kufilisiwa na kutaifishwa kila kitu pamoja na kuondolewa kabisa kwenye mfumo . Hii italeta uwajibikaji
 
Serikali dhaifu Ina mawazo dhaifu, watendaji dhaifu, machawa wenye akili dhaifu na hivyo kila kitu kinakwama.

Mleta mada yupo kwenye mnyororo wa udhaifu pia.

Kweli, haya ndio matokeo ya serikali dhaifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…