Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 95,871
- 116,627
Ni kada wa CCM hawezi kufanywa chochote
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Akiwa ni kada wa sisiemu anakuwa juu ya sheria ?Ni kada wa CCM hawezi kufanywa chochote
Hivi ni nani huyo asiyetajwa?Ana kadi ya chama huyo hakuna wa kumgusa
Kipindi jengo linajengwa serikali walikuwa wapi kuona kama halijakidhi viwango
Niaje waungwana
Kwa kile kilichotokea jana hapo K'koo, mimi nashauri kwanza mwenye ghorofa lililoanguka akamatwe, mali zake zifilisiwe, na kiwanja kilichokuwa na jengo kiuzwe ili hela zitakazopatikana zitumike kuwasaidia wale wote waliojeruhiwa na waliofiwa na baba zao, wame zao, wake zao, watoto wao nk.
Ni ukweli ulio wazi kwamba baada ya msiba huu wa taifa kuisha na kila mtu kuendelea na maisha yake, kuna ndugu zetu ambapo watabakia na ulemavu wa kudumu, kuna watu ambao watabakia mayatima baada ya kupoteza baba au mama katika janga hilo. Sasa watu wa aina huyo ni nani atakaewasaidia kuwasomesha, kuwalea, kuwahudumia nk.
Najua kwa upande wa serikali ni vigumu sana wahanga kupata msaada hapo baadae. Maana janga likishaisha kila mtu ataelekea ya kwake, hivyo waliofiwa na wazazi wao hawatopata msaada tena. Kwa nchi za wenzetu ile bajeti inayotengwa kila mwaka kwa ajili ya majanga ingetumika kuwasaidia waliokumbana na majanga hayo japo kwa kuwapa mitaji waathirika.
Lakini kwa nchini kwetu ndo hivyo tena, fedha za majanga zinaishia kutumiwa na viongozi fulani kwa kununua viwanja na kujenga majengo makubwa makubwa huko Mbweni, Salasala, Bunju nk.
Halafu yanapotokea majanga ya ghafla kama haya unakuta wanakuja na majembe pamoja na kuleo kuchimbia kifusi kizito cha tani zaidi ya 50. Kuna watu wameachwa yatima wengine wamepoteza viungo vyao kizembe kwa sababu ya tamaa ya mtu mmoja.
Hivyo huyo mtu aadhibiwe kwa kunyang'anywa kiwanja ili kuizwe na hela kupelekwa kwa wahusika, hii ikiwa pamoja na kutaifisha mali zake zote alizochuma iwe kihalali au kiharamu ili kufidia hasara aliyowapa wenzake hapa duniani na pia iwe fundisho kwa wapumbavu wengine wenye mawazo finyu kama yake.
Soma Pia: Ghorofa limeporomoka Kariakoo asubuhi ya leo Novemba 16
Ushauri mzuri kwa mamlaka na wahusika mbali mbali.
RIP kwa watanzania wenzetu wote waliokufa katika ajali hiyo. Na wale waliopata majeraha Mungu muweza wa yote awaponye.
Asanteni
Utakamatwa wewe kwa uchochezi na upuuzi wako na unyonge wako..period
Ana kadi ya chama huyo hakuna wa kumgusa
Hapa ndio pa kuanzia,then ijulikane nani aanze kukamatwa,mwenye mali au mamlaka husika...Kipindi jengo linajengwa serikali walikuwa wapi kuona kama halijakidhi viwango
Hadi sasa imeripotiwa idadi ya wenzetu wangapi waliotutangulia?
Kariakoo wange-replan upya hilo eneo matathalani hilo lingebaki eneo la wauzaji wa nguo pekee, maeneo mengine yaanzishwe kuweka watu wa bulding materials, stationeries simu na vifaa vyake ili mwisho wa siku maeneo muhimu mfano ya assembly point na disaster rescue access point ziwepo.
serikali ianzishe maeneo mengine ambayo yata serve kama Kariakoo lkn kwa bidhaa ambazo pekee zitakuwa zinapatikana maeneo hayo, so hata population itapungua maana wahitaji watakuwa wanaenda eneo specific kwa ajili ya kufuata huduma/ bidhaa zinazopatikana mahali hapo, Shida ss Kariakoo inayotokea ni kwa sababu eneo limekuwa centralised kwa bidhaa zozote wenyewe wanasema karikaoo kila kitu kinapatikana ifike mahala tuseme kariakoo ni kwa ajili ya bidhaa hii na ukitaka bidhaa hii nenda mahala pengine!!
Bima ndio itafanya kila kitu labda tu awe hakukatia hilo mengi bila na hilo litaondoka na wengi
Anaweza kuwa na vibali halali vya umiliki wa eneo, lakini sidhani kama anaweza kuwa na vibali halali vya kuchimba underground. Huyo alitumia uhuni kwa kuwahonga watu wachache kwenye mamlaka ili wamuache ajenge tu atakavyo. Sasa imekula kwake.
Majizi yote yapo CCMUchama unaliangamiza taifa nchi hii.
vip kuhusu ajali za barabani, majanga ya moto na ajali za boti majini, njaa, ukame , mafuriko n.k nani awajibishwe na kwa style ipi?🐒
Kuna mtu anataka kukukata kumbe!Ataekuja kunikata awe ameaga kabisa kwao. Maana atachokipata ataenda kuhadithia vizuri huko ahera.
Jaribu kusogea hapo uone, kama hayupo juu ya sheria mpaka leo mbona hajakamatwa?Akiwa ni kada wa sisiemu anakuwa juu ya sheria ?
Serikali dhaifu Ina mawazo dhaifu, watendaji dhaifu, machawa wenye akili dhaifu na hivyo kila kitu kinakwama.
Mleta mada yupo kwenye mnyororo wa udhaifu pia.