Nasikitika sana mkuu wangu 'peno hasegawa', kwani ni wazi hujui unachotaka upewe.
"Journa" ni kitu gani, na itahusiana vipi na Ph.D. ya huyo unayetaka kumlipua?
"Journal" haina uhusiano wowote na kiwango cha elimu alichonacho mhusika. Hata yule binti yako wa miaka 14, atakuwa na "Journal" (Diary), ambayo hatapenda wewe uisogelee karibu. Na wenyewe hawapendi kuiita "diary", bali 'Journal"
Maana nyingine ya "Journal" ni majarida yanayochapisha maandiko ya tafiti ya kitaaluma, wenyewe wanaziita 'papers'.
Hakuna taasisi yoyote ya elimu duniani inayo ainisha kiwango cha elimu ya mtunukiwa ikihusiana na "journal".
Inawezekana umechanganya "Thesis", au hata "Disertation" na hiyo "Journal."
Na kama unatafuta maandiko hayo niliyokuwekea hapo, basi njia rahisi ya kuyapata ni kwenda kwenye maktaba alikopata hiyo Ph.D. yake. Ni taratibu duniani kote kuwa na uhifadhi wa maandishi ya namna hiyo kwenye maktaba husika.