GE2025 Mwenye masikio na asikie sasa endeleeni kujidanganya kuwa mtazuia uchaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
57,035
Reaction score
46,479
Wanaukumbi.

Sina uhakika kama watu wengi hasa hawa washabiki wa wanaharakati wanaelewa uzito wa maneno haya kutoka kwa rais wa nchi. Sina uhakika kama wanaelewa anapofikia Rais wa nchi kutamka hivi wanaelewa nini kinatakiwa kufuata aunini maana yake kwa vyombo vya usalama vyenye jukumu la kulinda amani na usalama wa nchi hii.

Rais wa nchi yoyote ile ana jukumu la kulinda amani na utulivu wa nchi nyakati zote ndiyo maana Rais anaweza kuamuru vyombo vya usalama likiwemo jeshi kuingia vitani kupambana na nchi nyingine au vikundi ndani ya nchi vyenye kutaka kuleta uvunjifu wa amani na kuvuruga ustawi wa taifa na nchi husika..

Kama hili linaeleweka na nimejaribu kuliweka kwa lugha nyepesi sana ili lieleweke bila mikwaruzo ni wazi sasa huu ujinga mnaodanganyana sijui kuandamana kuvuruga na kuzuia uchaguzi sijui kukomboa nchi ni kitu cha hatari sana mnacheza nacho na mnajidanganya kuwa mtaweza kufanya.

Nimeona mahali eti watu wapige honi sijui wapige masufuria na upumbavu mwingi tu kama ishara ya kupinga sijui serikali na dola. Hivi mmeishiwa mbinu kiasi hiki mpaka sasa mnapiga masufuria na madebe ili kuleta kelele! Hivi mko sawa kiakili kweli au mnajipaga muda kusoma na kujisikiliza vitu mnaandika nyie watu?

Kwa hiyo kupiga masufuria na kupiga honi za magari ndiyo nini? Kwa hiyo kwa akili zenu wafuasi wenu wote wana magari au? Yaani wanapiga honi za magari gani au yapi?

Hizi ni mbinu za kijinga na kioumbavu sana na kama kwa kufanya haya mnadhani eti ndiyo mtakuwa mmefanikiwa kuzia uchaguzi na kupindua serikali basi jihesabieni kuwa ninyi ni watu wa jinga sana kwa kuwa mnawaza mambo ya kijinga na yasiyowezekana.

Tukirudi kwenye kauli ya Amiri Jeshi Mkuu ni kwamba amekula kiapo kuhakikisha nchi hii inakuwa na amani na utulivu sana na ni jukumu lake la msingi kuahakikisha Tanzania inakuwa salama.

kwa hiyo kama kuna mtu au kikundi cha watu hasa hawa wanaharakati kinadhani kina uwezo wa kuzuia uchaguzi na kuangusha serikali na sijui kukomboa nchi basi nawashauri wasikilizi mara kwa mara hii video yaani wasikilize kwa kujirudiarudia halafu mwisho wake wataelewa kitu wanacheza nacho na madhara ya kucheza nacho ni yapi!

WAZAZI wa Tanzania nawasihi sana mkishamaliza kula mkiwa mmekaa na watoto wenu wasikilizisheni watoto wenu hii video clip hata mara 3 hivi mpaka 5 kabla hawajakwenda kulala ili iwakae kichwani na wakiwa wanatembea kila hatua wanayokanyaga iwe inawapa mwangwi wa walichokisikia na kuwakumbusha hatari wanayodanganywa kuwa wanaweza kuifanya kwa kigezo cha kuzuia uchaguzi sijui kuandamana.

Hakuna Rais duniani atakaye kubali kuacha kulinda amani na utulivu wa nchi yake kwa kuwa hivho ndicho kitu aliapa kukilinda kwa nguvu zake zote na maarifa yake yote. Sasa kama kuna mtu anadhani anaweza kwenda mbele na kukinzana na kiapo hiki basi sisi tumetimiza wajibu wetu wa kuwakumbusha na kuwaambia kwa undani sana.

MWISHO ni kuwa aliye na masikio asikie haya mambo! MSIJE KUSEMA HATUKUWAAMBIA AU KUWAKUMBUSHA..
 
UFIPA KWANI MNATAKA NINI ? HEBU SEMENI BASI TUWASAIDIE!
 
Wahuni mnatapatapa kweli kweli. Mnajua fika yakitokea maandamano, maslahi yenu nayo yatafikia tamati.
 
Madagascar hawakua na Jeshi au yule Rais hakua Amirijeshi Mkuu suala ni kwamba Tanzania maisha bado ni rahisi sana hakuna Amirijeshi anaweza kushinda Nguvu ya Umma kwa taarifa Umma ndo wenye mamlaka ya Mwisho ya Nchi
 
UFIPA KWANI MNATAKA NINI ? HEBU SEMENI BASI TUWASAIDIE!
Ufipa au ni wananchi wenyewe na visirani vyao?

Umemwona nani mwanachama yeyote au kiongozi yeyote wa ufipa akihamasusha maandamano mkuu
 
UFIPA KWANI MNATAKA NINI ? HEBU SEMENI BASI TUWASAIDIE!

Sasa wewe Ritz unawasaidia kama nani.

Hata hivyo Madai yao waliyayaweka wazi toka mwanzo kwa nini unataka kuwasaidia dakika za mwisho .... Au na wewe tayari Mavi yanagonga Chupi...!!?
 
Wanaukumbi.

Sina uhakika kama watu wengi hasa hawa washabiki wa wanaharakati wanaelewa uzito wa maneno haya kutoka kwa rais wa nchi. Sina uhakika kama wanaelewa anapofikia Rais wa nchi kutamka hivi wanaelewa nini kinatakiwa kufuata aunini maana yake kwa vyombo vya usalama vyenye jukumu la kulinda amani na usalama wa nchi hii.

Rais wa nchi yoyote ile ana jukumu la kulinda amani na utulivu wa nchi nyakati zote ndiyo maana Rais anaweza kuamuru vyombo vya usalama likiwemo jeshi kuingia vitani kupambana na nchi nyingine au vikundi ndani ya nchi vyenye kutaka kuleta uvunjifu wa amani na kuvuruga ustawi wa taifa na nchi husika..

Kama hili linaeleweka na nimejaribu kuliweka kwa lugha nyepesi sana ili lieleweke bila mikwaruzo ni wazi sasa huu ujinga mnaodanganyana sijui kuandamana kuvuruga na kuzuia uchaguzi sijui kukomboa nchi ni kitu cha hatari sana mnacheza nacho na mnajidanganya kuwa mtaweza kufanya.

Nimeona mahali eti watu wapige honi sijui wapige masufuria na upumbavu mwingi tu kama ishara ya kupinga sijui serikali na dola. Hivi mmeishiwa mbinu kiasi hiki mpaka sasa mnapiga masufuria na madebe ili kuleta kelele! Hivi mko sawa kiakili kweli au mnajipaga muda kusoma na kujisikiliza vitu mnaandika nyie watu?

Kwa hiyo kupiga masufuria na kupiga honi za magari ndiyo nini? Kwa hiyo kwa akili zenu wafuasi wenu wote wana magari au? Yaani wanapiga honi za magari gani au yapi?

Hizi ni mbinu za kijinga na kioumbavu sana na kama kwa kufanya haya mnadhani eti ndiyo mtakuwa mmefanikiwa kuzia uchaguzi na kupindua serikali basi jihesabieni kuwa ninyi ni watu wa jinga sana kwa kuwa mnawaza mambo ya kijinga na yasiyowezekana.

Tukirudi kwenye kauli ya Amiri Jeshi Mkuu ni kwamba amekula kiapo kuhakikisha nchi hii inakuwa na amani na utulivu sana na ni jukumu lake la msingi kuahakikisha Tanzania inakuwa salama.

kwa hiyo kama kuna mtu au kikundi cha watu hasa hawa wanaharakati kinadhani kina uwezo wa kuzuia uchaguzi na kuangusha serikali na sijui kukomboa nchi basi nawashauri wasikilizi mara kwa mara hii video yaani wasikilize kwa kujirudiarudia halafu mwisho wake wataelewa kitu wanacheza nacho na madhara ya kucheza nacho ni yapi!

WAZAZI wa Tanzania nawasihi sana mkishamaliza kula mkiwa mmekaa na watoto wenu wasikilizisheni watoto wenu hii video clip hata mara 3 hivi mpaka 5 kabla hawajakwenda kulala ili iwakae kichwani na wakiwa wanatembea kila hatua wanayokanyaga iwe inawapa mwangwi wa walichokisikia na kuwakumbusha hatari wanayodanganywa kuwa wanaweza kuifanya kwa kigezo cha kuzuia uchaguzi sijui kuandamana.

Hakuna Rais duniani atakaye kubali kuacha kulinda amani na utulivu wa nchi yake kwa kuwa hivho ndicho kitu aliapa kukilinda kwa nguvu zake zote na maarifa yake yote. Sasa kama kuna mtu anadhani anaweza kwenda mbele na kukinzana na kiapo hiki basi sisi tumetimiza wajibu wetu wa kuwakumbusha na kuwaambia kwa undani sana.

MWISHO ni kuwa aliye na masikio asikie haya mambo! MSIJE KUSEMA HATUKUWAAMBIA AU KUWAKUMBUSHA..
Kama huyo unayemsema yupo kweli serious basi hadi sasa angekuwa keshaweza kuzuia mauwaji na utekaji unaoendelea nchini kwa kuwakamata hao wanaoitwa wasiojulikana, ila hajaweza kufanya hivyo na wasiojulikana wanateka raia mchana kweupe katikati ya umati wa watu na kwenda kuwauwa huku wewe unatuambia kuwa yeye aliapa kulinda amani na utulivu.

Sasa ni utulivu na amani ya nani hasa ambayo anataka kuilinda hiyo october 29 hali ya kwamba sasa hivi ndani ya nchi yake anayoiongoza wananchi wake kutekwa na kuuliwa imekuwa ni matukio ya kawaida tu? Mbona hatangazi vita kwa hao wasiojulikana ambao hufanya wananchi wake kukosa amani na utulivu?

Na ikiwa kwamba yeye anahusika na hayo matukio ya utekaji na mauwaji ya raia wake kwa kuwatumia hao wasiojulikana, hapo utasemaje kwamba kiongozi huyo anajali utulivu na amani? Ni utulivu wa nani anaotaka kuulinda hiyo oktoba 29?
 
Back
Top Bottom