Mwenye nguvu mpishe: Watu wa makundi haya hawagusiki kirahisi, wana nguvu kubwa sio wa kugombana nao utazama kwenye kina kirefu

Wateule wa Rais - Wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, n.k.

Watumishi wa vyombo vya ulinzi - Polisi, Jw, Usalama.

Wahindi na Waarabu

Watu wao wa karibu - watoto, ndugu, wazazi, marafiki wa karibu

Kama wabuduli hayumo humo uzi ni batili
 
umetunga ukiwa wapi ,mkuu
 
Kuna soja alipoteza jicho kisa mentality hizi hizi za untouchable. Kamuonea raia, raia akapima upepo akaona huyu mjeda simmudu. Akamvia kwenye pombe spoku ya jicho akapotelea wapi saivi.

Mmewahi kuua kenge? Kenye mkimtaitisha mkamuweka mtu kati na hana pakutokea, atakurupuka hapo anamvaa yoyote yule kati yenu mliyemuwekea duara achomoke.

Ndivyo ilivyo unavyomuonea mnyonge ukijihisi wewe ni untouchable.
Ni mpumbavu pekee atawaza kumchapa makofi IGP ikitokea ameonewa na hana njia nyingine ya kupata haki yake.
 
Huku mkoani kwetu kuna Muhindi mfanyabiashara mkubwa tu binti yake alipewa Mimba na kijana fulani hivi. Yule muhindi akachukua polisi akaenda kumuweka ndani yule kijana na akazuia dhamana.

Kilichotokea baba wa yule kijana kumbe ndio mkuu wa upepelezi wa mkoa. Alipopata taarifa akamweka ndani yule Muhindi huku akizuia dhamana. Wiki nzima alikaa ndani.

Kwa hiyo hakuna asiyegusika, usipoguswa na wa chini, utaguswa na wa juu yako.
 
Hii ilikuwa ligi nzuri, bila Shaka ma Dr. ndio walishinda
 
Haki yako ni yako mwenyewe haimuhusu mwengine.....

Yaani kwa kuwa wewe ni fulani ndio umuonee mwenzako ?!! 😲😲
Njia ziko nyingi za mapambano....nanyi vilinge hamvitaki....🤣
 
Pamoja na kwamba watu wote wana haki sawa, ulipotaja kuogopa wahindi na waarabu imethibitisha kabisa kuwa fikra zako ni mbaya na haziwezi kulisaidia taifa.
Tunahitaji kujenga fikra za watu wetu wajiamini, wapambane kulitetea taifa lao.
Hakika....

Huyo ana "slavery mentality".....

Iko hivi.....ukiwa na akili huwezi kumuonea mtu kwa sababu ya cheo ama nafasi uliyopo kwani inawezekana kabisa huyo dhaifu umuoneaye baba yake mdogo ndio mkuu wenu huko JUU....yako mengi hayo.....mengi mno.....

Binafsi ninayaheshimu mpaka majani ninayoyakanyaga njiani 🤣
 
Hayo yako mengi mno ...🤣

Muhimu tuthaminiane na tuheshimiane utu wetu ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…