Ni ngumu sana kumwelimisha asiyejua kuwa hajui kwani kila unapojaribu kumpa maarifa, yeye huzidi kuyaepa. Wengi wanaopinga kununua ndege kwa cash hawajui hata tofauti baina ya hizo arrangements. Yawezekana wanadhani ununuzi wa ndege ni sawa na ununuzi wa gari.
Ndege hununuliwa kwa order hivyo unapotoa cash unapata ndege haraka zaidi (miaka 1-2). Bali unaponunua kwa mkopo hukuchukua miaka mingi (mpaka 7) kutegemeana na backlog ya mtengenezaji.
Makampuni makubwa kama Emirates tayari yamejiimarisha hivyo hawahitaji ndege on short time basis hivyo huwa tayari kusubiri hata miaka 5 au 6 na ndiyo sababu hukopa.
Sasa siye tunahitaji kuamsha aviation sector now na si miaka kenda ijayo.
Pia gharama ya kukopa huwa kubwa kuliko cash. Kwa mfano. Sera ya uchakavu ya ATCL ni miaka 33 kwa kila ndege mpya. Kwa bei ya Bombardier Q400-8 ya 2016 ($31m), ikiwa wangenunua kwa mkopo/kukodi ingewagharimu mara 5 zaidi ya hiyo gharama kwa kipindi cha miaka 33 kwa ndege 1.
Tatizo hapa ni kuwa kila mmoja anajiona Transportation analyst na hivyo kudhani tunajua kuliko serikali.
Sent using
Jamii Forums mobile app