Mwenye Updates za Stiegler's Gorge, SGR na bomba la Hoima atupatie. Mbona kama mbwembwe zimepungua? Tunakwama wapi?

Mwenye Updates za Stiegler's Gorge, SGR na bomba la Hoima atupatie. Mbona kama mbwembwe zimepungua? Tunakwama wapi?

Hatujadili majungu! Tanzania ilikuwa kwenye hai mbaya sana wakati wa JK, rejea vigenerator kila kona, miradi ya kufua umeme kwa kuwakandamiza Watanzania nk. Wafanyakazi hewa wakati wa JK walishamiri, hata watoto wake nao walikuwa kama marais nk, Membe naye ambaye ni ndugu alitaka kubatiziwa urais what a shame! Waungwana hukaa kimya.

Mbwembwe nyiingi hata hela za kupambana na korona hamna mpk mchukue za kwenye mbio za mwenge.
 
Watz "wa mitandaoni" wa ajabu sana. Yapi Merkezi hutoa updates za SGRTz lots zote mbili kila mwezi kwa youtube. Pia TRC reli tv nao kila leo wana updates. Nyerere dam updates zake hutolewa na Tanesco yetu tv kule youtube.

Kisha kuna "mzalendo" anayetaka hizo info apelekewe kwa anwani yake ya posta anakuja na thread kama hii. Afrika kuna vituko vingi sana. Kuna mzungu aliandika kitabu: Vituko haviishi Afrika, kila siku kuna kituko kipya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mi nashangaa watu kupoteza muda wao kumjibu mtu kama huyu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Project ya bomba la mafuta ni project ya kitapeli. Museveni ni tapeli kama matapeli wengine. Magufuli alikuwa hajamjua vizuri Museveni ndio maana alidhani anaongea na mtu wa maana. Hiyo project ya Bomba la mafuta ilikuwa lipitie Kenya, baadae akaleta huo mradi Tanzania. Lakini mpaka leo hakuna linaloendelea na Museveni tayari wameshazenguana na wawekezaji wa hilo bomba.

Kimsingi hilo bomba Tanzania haitoi hata shilingi moja, zaidi ya kutoa njia ya kupitisha na kuwinda fursa za kiuchumi za ujenzi na uwepo wa hilo bomba. Mwanzo ilikuwa Magufuli anasifiwa kuwa ni sehemu ya mafanikio yake jambo ambalo lilikuwa ni upotoshaji wa wazi. Huyo Museveni tulisema ni tapeli tu, maana aliwahi kuitaka bandari ya Tanga enzi za Mkapa ili apewe sehemu aboreshe kwa ajili ya mizigo ya Uganda, na kweli alipewa, lakini hakuwahi kuleta hata tofali bovu. Hivyo deal la bomba la mafuta ni kama ishakuwa deal mfu, na usishangae akipitishia hilo bomba Kenya.
Stupid. hivi katika akili yako unajua mu7 ndio analeta bomba tz. bomba linaletwa na kampuni ya total. total ndio wenye visima uganda na wao ndio wanatoa $4 billion za kujenga bomba. na total ndio walimgomea mu7 kupeleka bomba kenya. hivi mbona mnashindwa kujua hata vitu raisi tu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna aliyesema kuwa reli haijengwi, bali muda tuliombiwa kuwa itakuwa tayari ili kusaka kiki, hauendani na kinachoendelea. Huo mradi wa SG nao umegubikwa na porojo nyingi, mwanzo hadithi ilikuwa tunajenga kwa fedha zetu za ndani, ghafla hadithi imegeuka tunakopa. Sasa kama tunakopa na mwanzo tulisema ni fedha za ndani, una uhakika gani na huo mradi kukamilika kwa muda tulioambiwa?

Cdm sio kwamba hawana ofisi, bali ni lini watakuwa na ofisi yenye hadhi ya chama chao. Hata Tanu walipokuwa wanataka uhuru, hawakuwa na ofisi yenye ghorofa 50, maana lengo ilikuwa sio kuwa na ofisi kubwa, bali kuleta uhuru. Jiulize ccm ilichukua muda gani kuwa na ofisi kama ya Dodoma , huku ikiwa imezaliwa ikiwa madarakani.
umeishia darasa la 7 nini mkuu. hujui kama kwenye proect planning kuna kitu kinaitwa delay. wewe unajua duniani kila project ikipangwa inaenda exactly kama ilivyopangwa. ndio maana jf hua naingia mara moja moja sana siku hizi maana wajinga ni wengi mno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
stupid. hivi katika akili yako unajua mu7 ndio analeta bomba tz. bomba linaletwa na kampuni ya total. total ndio wenye visima uganda na wao ndio wanatoa $4 billion za kujenga bomba. na total ndio walimgomea mu7 kupeleka bomba kenya. hivi mbona mnashindwa kujua hata vitu raisi tu


Sent using Jamii Forums mobile app

Ficha ujinga wako we dogo, hayo mafuta yako kwenye nchi ya Total au Uganda?
 
Ficha ujinga wako we dogo, hayo mafuta yako kwenye nchi ya Total au Uganda?
huna unachokijua bora ukae kimya. wewe unajua hii mikataba inaingiwa vipi. waambie basi hao uganda na mu7 watoe hizo $4bilioni wajenge bomba. mu7 na kenyatta walikuwa washasign MOU. lakini total akakataa akasema anataka bomba lienda tz na si kenya na imekuwa hivyo. kaa kimya ufiche ujinga wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nani amekwambia limegeuka hewa. mu7 alivyokuja Tz mwaka jana ulimsikia JPM alimwambia nini mu7? au ulikuwa huelewi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Politics my dear .Je ne crois jamais aux paroles sans actions. Je suis scientifique,J'observe et j'analyse ce que je vois,les choses réelles. Pas de paroles sans fait .
M7 aliambiwa akafukuze watendaji wake uliona kafanya hivyo?
Total walijitoa,uliona wamerudi ?
Je ne suis pas politicienne,je m'appuie aux facts et pas au parole vide.
 
Hakuna mradi ambao ujenzi umesimama.miradi haijakamilika lakini ujenzi unaendelea. Niko mita 100 eneo la mradi SGR.ni suala la muda tu.kila kitu kitakamilika. Na nyinyi mjenge makao makuu ya chama..tutawachangia kama tulivyowachangia viongozi wenu wakiwa mahabusu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na sisi tunasubiri tujengewe kama nyie mlivyojengewa na wachina hapo Lumumba pamoja na mabilioni mnayoyapata tena miaka zaidi ya arobaini!!
 
Mafuriko yaliyotaka kubomoa daraja la mto Ruaha wiki iliyopita pale Kidatu na kufurikisha vijiji kadhaa yameleta dhahama eneo la tukio la ujenzi wa steigler's gorge.
 
Mtashindwaje kufurahia Miradi endapo itashindwa kuendelea ikiwa tu mnaombea Hadi Corona ije ili Hali inakuja kuchezea vichwa hata vya vitoto vyenu na Wala haitabagua Vyama??

Mbuzi kasoro mkia ninyi!!!
 
Cha ajabu ni kwamba, wao kwenye ilani Yao kulikuwepo hiyo ya ununuzi wa ndege, sijui walikuwa wakimanisha watanunua ndege Aina ya kunguru?

Wenzetu ijapokuwa ni watu wazima Ila wamejilazimisha wawe watoto, hawana kumbukumbu tena kipindi hicho walikuwa wakihitaji nini na walikuwa wakinadi nini
Sahihi kabisa. Kabla ya 2015, miongoni mwa mambo ambayo tuliyapigia sana kelele ni ATCL kukosa uhai na hivyo seeikali kushindwa ku-effect uchumi kupitia sekta ya usafiri wa anga. Hali ambayo ilipelekea uhai wa sekta hiyo kutegemea mashirika yasiyo na malengo/mikakati ya kudumu (rejea Community Airlines, Fast Jet) kitu ambacho kisingewahi kuusaidia uchumi wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama unashauri kila kitu twende you tube JF ya nini sasa, mind you mtu anapouliza swali public inawezekana si kwa faida yake pekee ni faida kwa wengine pia.
Soma vizuri nilichoandika mzazi. Hapa hapa JF kuna thread yenye live updates za SGRtz. Kudhani kuwa publicity au coverage ya hii miradi itakuwa sawa wakati wa uzinduzi na wakati wa utekelezaji ni kuwa na matarajio makubwa mno.

Bali ni sisi ambao si wafuatiliaji wazuri wa miradi yetu pindi ambapo publicity yake haiko juu. Hii ndiyo sababu hata hapa JF, thread ambayo itampatia msomaji taarifa nyingi kuhusu SGRtz kwa mfano, iko "Kenyan News Forum"!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom