Kumbe atajwe nani kama siyo rais Magufuli, anaetumbua watumishi ni nani?
Mleta hela za barabara, maji, umeme, matundu ya choo, flaiova, sgr ni nani?
Msema kweli mpenzi wa Mungu ni nani?
Asiyepangiwa mambo na rais anaejiamini ni nani?
Asieleta "chakura" wakati wa njaa ni nani?
Aliyemwambia yule mama "shida yenu ni kupanuliwa tu" ni nani?
Mleta Noah kwa kila mtanzania ni nani?
Aliyesifiwa kwa kuleta kupatwa kwa jua Mbeya ni nani?
Sasa asipotajwa yeye atatajwa nani?
Hata kina Rungwe na Lipumba wanamtaja huyo huyo, haiwezekani kufanya kampeni bila kumtaja rais aliyepo madarakani na chama chake kwenye kampeni haiwezekani Dunia nzima.
Lazima atajwe kwa mema au mabaya yake, hivyo wana ccm vumilieni yote haya yatapita.
"Sifa na kuabudi zinatusubiria Mbinguni" lakini kutajwa hapa Duniani atatajwa sana na bado.
Sent from my TECNO K9 using
JamiiForums mobile app