Mwenyekiti atishia kwenda kwa Rais mbele ya Waziri Lukuvi

Mwenyekiti atishia kwenda kwa Rais mbele ya Waziri Lukuvi

Ukiitizama hii video kwa makini ukiwa neutral kabisa utagundua huyo mwananchi ana changamoto kidogo ktk akili yake,hana utulivu kabisa.
Ndg Lukuvi alipaswa kuwa mtulivu kwa kuliona hilo angeahirisha kumsikiliza kwa kumuambia tu kwa utulivu wewe jambo lako ni zito tuonane pale ofisini.

Akija ofisini unachukua mabarua yake hayo unamuambia kaa hapo kunywa chai usizungumze,unazisoma ukielewa unatoa uamuzi.
Uongozi ni pamoja na uvumilivu wa kumudu personality za Watu.
Waziri amekosa hekima na busara amebomoa ajajenga pale
 
Huyu mwananchi amemdharau sana Lukuvi, na kaongea kishari shari sana.

Haya ndiyo matatizo ya dikteta kuhodhi madaraka yote. Wananchi wanaanza kuwaona mawaziri kama takataka tu.

Mitano tena!
Yeah hii nikweli inaanza kuonekana wa2 wamebaki kuamini kile tu anachosema Rais na sio wasemalo mawaziri
 
Huyu mwananchi amemdharau sana Lukuvi, na kaongea kishari shari sana.

Haya ndiyo matatizo ya dikteta kuhodhi madaraka yote. Wananchi wanaanza kuwaona mawaziri kama takataka tu.

Mitano tena!
tatizo sio mwananchi, tatizo ni Lukuvi katika hiki tulichokiona. Yule mwananchi ni mwajiri wa Lukuvi, kwanini Lukuvi kakaa kibosi bosi badala ya kumvumilia bosi wake aeleze tatizo lake? Kisaikolojia yule mwananchi ni mwathirika (labda wa mambo mengi), Lukuvi alipaswa kumvumilia tu angemwelewa!
 
Badala ya kutoa hoja anaishi kwa nyota ya babu yake muasisi wa Tanu. Kwanini asingeleta hoja yake kwa staha?

Hatapata kitu hata akienda kwa JPM kama anadharau wasaidizi wake
 
Sikuwahi jua huyu waziri ana kiburi na dharau hivi. Khaaah.
Rais amtumbue huyu waziri hafai kabisa.
Afu anajibu kijeuri "nenda kamuone rais" jamani hata mshipa wa aibu hana.

[emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka huyo mama anamlazimisha mlinzi amtoe nje huyo m/kiti,
M/kiti nae anajibu "wee mama usiseme hivo je angekua rais hapa unaweza sema hivyo?"
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
mkuu kila nyuzi nakukuta...Hatari
 
Naye lakini ana kosa, kwa nini aanze kutambia uasisi wa babake? Kwani kama angeeleza kwa staha ingekuwaje?

..hiyo ya kumtaja baba yake nadhani ni kutokana na usumbufu aliopitia, na machungu aliyokuwa nayo.

..na pia anataja uasisi wa baba yake kwasababu ardhi "iliyodhulumiwa" ilikuwa mali ya muasisi.

..nadhani mlalamikaji alitaka kuonyesha jinsi watu wanaodhulumu walivyoota "mapembe" kwamba hawaogopi mali za mtu yeyote yule.

..binafsi sielewi kwanini Waziri Lukuvi alichukia baada ya mlalamikaji kusema yeye ni mtoto wa muasisi wa tanu. kwa kweli I dont see anything wrong kwa mtu kuwa mtoto wa muasisi. Sio dhambi.

..kingine kilichoonekana kumkera Waziri Lukuvi ni mlalamikaji kumtaja Edward Lowassa kwamba aliwahi kulitolea maamuzi suala lake. Inawezekana Waziri Lukuvi alidhani Edward Lowassa bado yuko Chadema.
 
Ukiitizama hii video kwa makini ukiwa neutral kabisa utagundua huyo mwananchi ana changamoto kidogo ktk akili yake,hana utulivu kabisa.
Ndg Lukuvi alipaswa kuwa mtulivu kwa kuliona hilo angeahirisha kumsikiliza kwa kumuambia tu kwa utulivu wewe jambo lako ni zito tuonane pale ofisini.

Akija ofisini unachukua mabarua yake hayo unamuambia kaa hapo kunywa chai usizungumze,unazisoma ukielewa unatoa uamuzi.
Uongozi ni pamoja na uvumilivu wa kumudu personality za Watu.
ni chizi huyo namjua vizuri sana nishakaa naye sana villa park
 
Definitely Lukuvi ana interest katika hilo eneo lililo porwa ndio maana alikuwa anakataa kusikiliza, ni aibu sana, kama alikuwa hayaki kusikiliza wananchi ilikuwa hana haja ya kuwaona
 
MTU ana Jazba ya kuona kuwa anadhulumiwa, waziri alipaswa kuwa Humble na kumvumilia Mwananchi na angempa muda Wa kumsikiliza ili amwelewe.

Badala yake nilichoona ni Waziri anajimwambafai tu, ila Hamna kitu kabisa..
Hivi hiyo sura ni ya kudhulumiwa?. Binadamu wanajitoa ufahamu kipindi hiki. Ni sawa na yule mama wa Tanga. Alilia machozi yakatoka kumbe Tapeli.
 
Huyo mzee ana matatizo sasa akisema yeye ni mtoto wa Muasisi ili aonewe huruma ama nini?

Kiufupi amekosea timing na anaonekana mjivuni
 
Huyo jamaa kamfuata Waziri kulalamika kwa sababu huko chini kote kaona hajapata haki.

Kuna tatizo ikiwa nchi mtu hapati haki mpaka aonane na waziri au Rais.
Miaka ya nyuma kidogo nilikwenda Tanesco wakati bado wapo pale ntuma ya samora avenue station au kama unaenda Police central, nilikwenda kumuona ofisa mmoja kwa ajili ya kunifungia Luku nyumbani.

Mule ofisini nilimkuta waziri wa nishati na madini Daniel Yona kabla hajapewa wizara ya Fedha, kwamba yeye ndio Boss wa Tanesco, na pale alukwenda personal kwa issue za umeme nyumbani au kwenye nyumba alizokuwa anajenga.

Baada ya Daniel Yona kutoka tu kwenye ile ofisi niliingia mimi na yule ofisa akawa na tabasamu bashasha kwangu akaniambia achana na wanasiasa hawa maneno matupu hata pesa ya chai hatoi blabla tu.

Mimi nikatowa mshiko pale nijampa akanipa mafundi na gari na vifaa vyote, yule Daniel Yona ilibidi asubiri mimi Pangu Pakavu kazi yangu ifanywe kwanza ndio wamfikirie yeye.

Kwahiyo tangu siku ile nilijufunza kitu kikubwa sana.

Sikushangaa hata kidogo Mkapa na Sumaye kushabikia rushwa na kuita takrima.

Walioiharibu nchi hii kwa kiasi kikubwa ni Mkapa na Sumaye, mnachokiona sasa hivi ni damage control tu.
 
Vitu vidogo kama hivi upunguza cv ya mtu kwenye jamii.Ni Kazi kubwa Sana kuijenga cv ni rahisi kuibomoa siku moja.
 
Back
Top Bottom