Mwenyekiti atishia kwenda kwa Rais mbele ya Waziri Lukuvi

Duh!
Eti nitaenda kwa raisi maana yake unamuona Waziri si chochote [emoji2960]
 
Jamaa ana kiburi. Utoto wake wa mwasisi unatuhusu nini sisi? Angesema tu mimi ni mwananchi mwenye tatizo ABC. simple like that. But kujimwambafy kwingi na mikwara mwishoni anaonekana anafanga fujo. Na anaonekana amesoma. You hit the point. Then unapoulizwa maswali mengine ndo unatoa maelezo. Unaposema mwenzako XXX alisema au alifanya hivi. Unakosea pia. Huyu ni Lukuvi na yule ni lowassa. Hapa hata kama humpendi Lukuvi ila si sahihi mtu adhalilishwe hivi kwa kisingizio cha utoto wa mwasisi. Asonge mbele.
 
Hana adabu Yule mzee kabisa, lukuvi angemsaidia ningeshangaa sana ,eti mwenzako kah,
 
Supreme power ya waziri haionekani
Nadhani kuna gap mihimili isije kuingiliana hapa
Yeye anasema rais hajui kuwa waziri anamwakilisha rais
 
Huyu mwananchi amemdharau sana Lukuvi, na kaongea kishari shari sana.

Haya ndiyo matatizo ya dikteta kuhodhi madaraka yote. Wananchi wanaanza kuwaona mawaziri kama takataka tu.

Mitano tena!
hapana zile ni hasira mkuu.
imagine mtu unaendesha kesi kwa miaka 30 bado unapigwa danadana tu lazima ujitoe ufahamu.
 
Nadhani Waziri kakosea, alipaswa awaachie hata wasaidizi wake waongee naye.

Shida Waziri anataka sifa kwa rais, ndio maana anataka majibu rahisi tu kwenye kamera aonekane katatua shida, mambo yakiwa na mkanganyiko kidogo ana panic. Raia nae anaona kabisa huyu Waziri hawezi kunisaidia mpaka niende kwa rais. Na pengine labda anajua historia fulani kuhusu huyo waziri katika miaka yake 30 ya kupambana na hiyo kesi.
 
ile ni jazba ya kudhulumiwa haki na inaweza kumkuta mtu yeyote.
Imagine leo hii uambiwe nyumba unayoitegemea kuishi inatakiwa ibomolewe pajengwe soko,au udhulumiwe uambiwe hustahili kukaa hapo.
Lazima ufahamu uruke mzee baba usifanye masihara
 
Eti mtoto wa muasisi wa TANU that's nosense...!!?
wazili anamwambia aende kwenye point yy analeta longo longo na jazba utadhani lukuvi ndio amempora ardhi?
ningekuwa mm ndio waziri huyo Bwana majazba ningemtandika kibao cha usoni...
 
uko sahihi kabisa mkuu,ilikuwa ishu ndogo sana.
Mtu ukishamjua ana matatizo mpe kichwa atatulia tu.
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]uko kama mimi aisee
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]walikutana pipa na mfuniko
 
Haijalishi bado anahaki ya kusikilizwa sio kupuuzwa

Watu hatufanani na uasili hatufanani pia.

Kila mtu ana haiba na silika yake.

Huyu ndivo alivoumbwa.
Jee, hiyo haki ya kusikilizwa inatokana na yeye kuwa mtoto wa muasisi wa TANU akiwa na Nyerere? Ina maana watoto wa watu wa kawaida tu wasisikilizwe? Hili ndilo suala lililomghasi Lukuvi akadiriki kumpa nafasi mlalamikaji mara tatu ajikite kwenye tatizo lake. Mlalamikaji alishindwa mara zote tatu na ndipo Lukuvi akaamua kuachana naye. Nakubaliana na uamuzi huo. Tusisikilize mtu kwa kuwa tu yeye ni fulani bali tuangalie tatizo lenyewe.
 
Huyu mwananchi amemdharau sana Lukuvi, na kaongea kishari shari sana.

Haya ndiyo matatizo ya dikteta kuhodhi madaraka yote. Wananchi wanaanza kuwaona mawaziri kama takataka tu.

Mitano tena!
Tulianza na msemo wa serikali ya viwanda,ilipoishia hatujui hadi leo. Ikaja serikali ya Magu , ikaja serikali ya mi tena, hatujakaa sawa sawa ikaja serikali ya kujifukiza! Kwa sasa tupo kwenye serikali ya makaripio mipasho na onyo. Full comedy.
 
huyo mhe. lukuvi nae si msikilizaji mzuri huyo mzee anakitu sema namna yk ya uwasilishi ni mzunguko ...aende tu huko kwa rais πŸ˜› πŸ˜› πŸ˜›
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…