Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi, Iddi Kimanta, amewataka vijana nchini kuwa na uchungu wa kukilinda na kukitetea chama hicho, huku akionya dhidi ya tabia ya kubeza au kuwasema vibaya viongozi waliopitishwa na vikao halali.
Akizungumza leo, Februari 3, 2026, katika kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa CCM lililofanyika Kata ya Ibindi, Halmashauri ya Nsimbo, Kimanta amekemea vitendo vya baadhi ya wanachama kugeuka na kuwashambulia viongozi ambao wao wenyewe walishiriki kuwapitisha kupitia kamati za maamuzi.
Mwenyekiti Kimanta amesisitiza kuwa nidhamu ndiyo nguzo ya chama, na amewataka vijana kuacha tabia ya kuwa wasemaji wa viongozi wasiofanya kazi vizuri (wazembe) kwani kufanya hivyo kunaharibu taswira ya CCM mbele ya umma.
Mbali na masuala ya kisiasa, Kimanta alipokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Ibindi. Mradi huo unatajwa kuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi wa Halmashauri ya Nsimbo, kwani utaleta huduma muhimu za afya karibu na makazi ya wananchi, ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Chanzo: Jambo TV