Pre GE2025 Mwenyekiti CHADEMA Mbeya: Tutamlazimisha Mbowe agombee Uenyekiti

Pre GE2025 Mwenyekiti CHADEMA Mbeya: Tutamlazimisha Mbowe agombee Uenyekiti

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mzee Mbowe anayo miaka zaidi ya sitini ,wapuuzi wana
Wakuu,

Tunaendelea kumywa mtori tukifiatilia hili kwa karibu. Bado ni mbinu ya kuichanganya CCM??

====

View attachment 3175976

Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya Masaga Kaloli, amesema anaamini bado Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho Taifa Freeman Mbowe ana nguvu za kukitumikia chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa Desemba 13, 2024, Masaga amesema Mbowe amepambana kukifikisha Chama hicho mahali kilipofika na kueleza kuwa yuko tayari kuongoza mchango wa kumchukulia Mbowe fomu ya kugombea na kwenda kumshawishi agombee uenyekiti.

Pia soma: Tundu Lissu atangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti CHADEMA

“Mimi kama mwenyekiti wa mkoa wa Mbeya nilitamani ningepata hata muda nikamwombe Freeman Mbowe, naye pia aingie kwenye kinyang'anyiro cha kugombea, ninatamani mwenyekiti aliyepo aendelee kuwa mwenyekiti kwasababC bado ana nguvu za kukitumikia hiki Chama na chama chetu cha upinzani kinahitaji watu, sasa leo hii akaastafu akawe kama mzee Mtei ni jambo la utani, Mbowe ndiyo kwanza bado kabisa, huwezi ukamwita Freeman Mbowe mzee", ameeleza Masaga.

Hata hivyo kiongozi huyo amesema anaona nafasi ya Tundu Lissu kuongoza chama hicho kwa siku za usoni lakini siyo kwa sasa akidai Mbowe bado anahitajika na wanachama walio wengi ili kukijenga zaidi chama hicho.
Mzee Mbowe anayo miaka zaidi ya sitini ,hapa mjinga mmoja anataka kutuaminisha kuwa huyu mzee ni KIJANA🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Mtoto wa ndesamburu na wifi yake ni wabungr wa kudumu wa Mzee Mbowe
 
Hawa Bawacha na huyo mwenyekiti wa chadema mkoa wote wanazingua. Taasisi haipaswi kuweka Msimamo wa kumuunga mkono mgombea fulani. Ikitokea Mnyika, Lema na Sugu nao wakivuta fomu je, itakuwaje? Watamuunga mkono nani na wamuavhe nani?
Chadema sio taasisi bali Lissu ndio anaenda kuifanya kuwa taasisi kwa maana mzee Mbowe kafanya cdm kama kampuni yake binafsi
 
Back
Top Bottom