Mwenyekiti, Katibu Mkuu CHADEMA kigugumizi cha nini sakata la Wabunge wa Viti Maalum?

Kama wameenda kinyume na chama wafukuzwe wameweka.mbele matumbo yao kuliko maslahi ya chama
 
Mnahangaika sana, Chadema ni taasisi imara. Alikuwepo Zitto, alipotoka mlifikiri Chadema itakufa. Alikuwepo Dr Slaa, apoondoka mlifikiri Chadema itakufa.
Wakati wa Zito chadema ilikuwa na wabunge wangapi na leo ina wabunge wangapi?
 
Lakini Kwa upande mwingine ni baraka! Kule bungeni ni kati ya viwanja vinavyoitaji watu wetu!
 
Since day one, those guys engender so much fear of Covid-19. Sasa ulivyoiweka kwenye title ndiyo kabisa umechochea fire & fury.
 
hizo sifa zote ulizowapa hao mabinti zimeyeyuka kama barafu kwenye jua since wameamua kukumbatiana na shetani.

Wamekwenda na maji tayari hao.
 
Baada ya Mheshimiwa Halima Mdee kula kiapo cha Ubunge kupitia viti maalum,alitoa shukrani kwa chama chake na Kwa Mwenyekiti wake Freeman Mbowe.

Sasa katibu mkuu wa chama mheshimiwa Mnyika alitakiwa ajue kusoma katikati ya mistari (read between lines) kwamba Mbowe hakutajawa na Mheshimwa Halima Mdee kwa bahati mbaya.Na Halima Mdee alionekana anaongea kwa unyenyekevu mkubwa jambo ambalo sio kawaida yake.

Sasa mimi naona mheshimiwa Mnyika ninaamini yupo vizuri na anayaona mambo kwenye 'three dimension' na ameshaamua liwalo na liwe.
 
Mnyika anajaribu kuwaaminisha wadanganyika/wadangaji wa nyikani kuwa Halima Mdee na mumewe wanaweza kwenda kula kiapo bila kushauriana na wenye chama(wachaga)
 

Ok
 
Dah....wakati wewe unawaza misimamo thabit....Dijei anawaza ELA [emoji2960][emoji23][emoji23]
 
Mbowe ana biashara zake za kusimamia, J J Mnyika anatosha!

Ya CDM yanawahusu vipi mboga mboga?

Hii wanaitaga "poking of noses onto issues of no concern to yourselves," yaani "kupiga chabo" kwa Kiswahili.

Hiiii bagosha!
 
Kuweka misimamo wazi siyo kuropoka.

Kwamba kuna mbunge bungeni na haafikiani na msingi mkuu wa chama kuhusiana na haramu ya uchaguzi wa 2020, kumlea huyo ni kulea kansa.

"If you disobey you go."

Hiyo si kuropoka. Huo ni msimamo thabiti!
2010 Chadema wakiwa na Slaa waliyakataa matokeo ila Mbowe,Lema,Mnyika,Sugu wakaenda bungeni.2015 wakiwa na Lowasa hawajakubali pia matokeo lakini kwa bashasaha na kina Heche ndani walitinga bungeni.2020 hawajakubali matokeo tena ila cha ajabu wanawazuia Bawacha wasiende bungeni!!
 

Mkuu kwa kauli hii ni kuwa mlizowea kuiiba mkijua kuwa watakwenda tu bungeni. Au siyo? Sasa mnashangaa kuwa ndiyo pori jipya, lakini nyani si wale wale?

Yaani kukwiba mmekwiba Ila tu hamtakaa mkiri ng'o! Au siyo.

Kwa taarifa yenu hii ngoma safari hii ni tofauti sana: Sasa basi! Ukipenda "safari hii hatutaki ukhanithi!"

Mliyoyategemea imekuwa ndivyo sivyo.

Wizi huu mbona utawatokea puani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…