The Burning Spear
JF-Expert Member
- Dec 23, 2011
- 4,118
- 9,864
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya momba, Mathew Chikoti, akinyeshewa na mvua wakati wa ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari Naming'ongo, na kuagiza mhandisi kuhakikisha ujenzi wa shule hiyo unakamilika haraka.
Ziara hiyo ilikuwa chini ya kamati ya fedha, uongozi, na mipango, ikiwa na lengo la kufuatilia maendeleo ya ujenzi na kuhakikisha shule inakamilika kwa wakati ili kutoa huduma kwa wanafunzi wa eneo hilo.
Kukamilika kwa shule ya sekondari Naming'ongo kutawapunguzia wanafunzi wa vijiji vinne changamoto ya kutembea zaidi ya kilomita 10 kwenda shule ya sekondari Chitete. Ujenzi ulianza tarehe 4 Agosti 2023 na ulipaswa kukamilika tarehe 30 Oktoba 2023. Hata hivyo, mradi haujakamilika kwa wakati kutokana na mkandarasi kusuasua. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Momba, Mathew Chikoti, amemwagiza mkandarasi kuongeza mafundi na kufanya kazi usiku na mchana ili mradi huo ukamilike kabla ya tarehe 30 Januari 2024.