Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Ni ziara kwenda kumuhadaa, kumkejeli na kumkashifu mwenyekiti huyo wa zamani, lakini pia huenda ikawa ni ziara kuchochea na kuzidisha kutwezana utu kama ambavyo kulifanyika kabla ya uchaguzi na kuzidisha migawanyiko na mpasuko zaid baada ya uchaguzi.
Dhihaka zinazotolewa na wasaidizi wa mwenyekiti mpya dhidi ya wa zamani, mathalani kwa kutokuwepo sherehe ya makabidhiaona ya ofisi, ni wazi zina baraka za mwenyekiti huyo mpya wa CHADEMA Taifa.
Wasaidizi hao wamefikia hatua hadi ya kusingizia kwamba mwenyekiti wa zamani kaondoka na kung'ang'ana na baadhi ya asset mbalimbali za chadema, kitu ambacho si kweli, lakini wanaona haitoshi, wanapanga kwenda kumdhihaki mpaka nyumbani kwake na familia yake.
Hii sio dalili nzuri hata kidogo, bali ni dalili ya kushindwa uongozi mapema hata kabla hali ya uhasama, vita vya maneno na uadui miongoni mwa zilizokua kambi za uchaguzi wakati wa uchaguzi wa chadema Taifa hazijatulia na kufanya maridhiano..
Ni kwa kiasi gani unaridhishwa na uongozi mpya wa upande moja wa chadema mpka sasa?🐒
Mungu Ibariki Tanzania