TANZIA Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Abraham Mengi afariki dunia akiwa Dubai, UAE

Aisee! Very sad news!
Loh!
Kapotea mtu muhimu Sana katika taifa hili.
 
Jamani! jamani! kifo hakina huruma daaah! Reginald Mengi uligusa Maisha ya Watanzania wengi, inasitisha, inahuzunisha lakini fikra na mawazo yako, wema wako utaendelea kuishi milele. Tangulia nami nimeamua kukufuata kwa kamba ya maombi niungane kukuombea, upumzike kwa raha na Amani katika Udongo mzuri!
 
Pumzika kwa Amani mzee wetu Reginald Mengi. Poleni sana Regina, Jacquline na familia yote kwa ujumba
 
Ndo hapo mkuu na mm nashangaa, hata gazet la nipashe la leo halijaandika hiyo habar

Siku zingine kama hujui Jambo Kwanza uliza Kuliko ' Kukurupuka ' katika Kulaumu. Magazeti mengi huwa yanakuwa tayari Kuchapishwa kati ya Saa 3 hadi Saa 5 Usiku na mengi mida hiyo hiyo ndiyo huwa yanakuwa yanasafirishwa kuelekea Mikoa na maeneo mbalimbali ya nchi. Mzee Mengi kwa mujibu wa taarifa amefariki Saa 7 usiku wa Kuamkia leo kwahiyo ulitaka Wahariri au Mhariri Mkuu awapigie Simu Madereva wote waliobeba Magazeti kuyapeleka Mikoani ambao wengine walikuwa wapo Chalinze na wengine Dumila na baadhi yao wakiwa ndiyo wanapandisha Mlima Kitonga wageuze haraka warudi Dar es Salaam ili wayashushe yawekewe hii taarifa kisha waanze tena Kuyasafirisha huko? Hivi unajua maana ya Vyombo vya Habari vingi Siku hizi kuwa na Kurasa zao za Mitandao mbalimbali ya Kijamii kama Facebook, Instagram na Twitter? Hii taarifa ni kweli haipo katika Gazeti la Nipashe la leo ila katika Mtandao wa Nipashe ipo tokea muda tu.

Hivi Watu wengine wakati Mwenyezi Mungu ' anatubariki ' wengine ' Akili ' Kubwa nyie wengine mlikuwa wapi hadi mnakuwa wa ' hovyo hovyo ' hivi?
 
R.I.P Mzee Mengi
Pole kwa Familia nzima!..
 
Apumzike kwa amani kwakweli..ametimiza majukumi yake mengi kwa watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…