Uchaguzi 2020 Mwenyekiti NEC: Uteuzi wa wagombea Urais utafanyika tarehe 25/08/2020 kwa wale wenye Sifa!

Uchaguzi 2020 Mwenyekiti NEC: Uteuzi wa wagombea Urais utafanyika tarehe 25/08/2020 kwa wale wenye Sifa!

Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Jaji Kaijage amesema uteuzi wa wagombea Urais wa JMT utafanyika tarehe 25/08/2020.

Jaji Kaijage amesisitiza kuwa ni wagombea wenye sifa ndio watakaoteuliwa kuwakilisha vyama vyao kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.

Chanzo: ITV habari!
Uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji wa mwaka 2019 ulikuwa na mikakati ya kishetani yenye viashiria vyote kama hivi. Hivi kweli tume inataka kwa makusudi kabisa kuliingiza taifa letu ktk mtanziko wa kisiasa usiokuwa na tija namna hii!

Hivi tume inataka kujipa mamlaka ya kutaka kuengua baadhi ya washindani halisi wa nafasi ya urais kupitia tu hofu ya mwenye madaraka ya juu ya uongozi wa nchi yetu? Hivi anajiamini kabisa ktk kubebwa kupitia mbeleko la vyombo vya dola kama hakikisho lake la kubakia madarakani kwa njia iwayo yoyote ile?
 
Kama mtu hana sifa kwanini wakampa fomu?

Kwani inawezekana chizi siku moja akaenda kuchukua fomu ya Urais wakampa?

Huyo jaji aache kuchezea akili za watu, tumeshajua mgombea wetu ni nani na kura zetu anazo, yeye na hayo matamko yake ya ajabu ajabu anajifurahisha tu.
Kama mgombea wenu Ana sifa wasiwasi wa nini? 🤣
 
Na hili la wagombea wenye sifa walisisitize sana maana wagombea wengine hawana ADABU kabisa.Mmoja wao ni yule anayesisitiza wananchi waingie barabarani kama atashindwa.Huyu sifa hana.
Halafu anagombea wakati yeye mwenyewe hayumo kwenye daftari la wapiga kura.
 
Ndiyo maana mara zote nashadidia dhana ya kurejea Mambo,(streamline) iwe Sheria nk ili kuondokana na dhana ya kufanya Mambo ambayo ni out of touch. Au ukipenda yasiyo na mashiko na kwenda na wakati( Relevance).

Kwa nini tume itoe fomu kwa mgombea, aanze kujinadi, atafute wadhamini nchi nzima, aanze kuaminisha watu juu ya ugombea( candidacy) yake.

Alafu Mwisho wa siku atangazwe kuwa hakukidhi sifa. Hata Kama hiyo Ni Sheria Basi Sheria hiyo ni ya kizamani na haiendi na wakati. ( It is draconian and irrelevant). Kwa nini hiyo tume isimfute( disqualify) mgombea Mara anapokwenda chukua fomu? Maana mwishoni Ni haohao waliotoa fomu ndo wataoa maamuzi ya aidha kufaulu(qualify) au la!

Hapo unakuwa tayari umemfanya huyo aliyeonyesha Nia ya kugombea kuwa amepoteza pesa, nguvu, na matumaini kwa ujumla. Sheria za namna hii ndo zinatakiwe zirekebishwe maana hata kiusalama tu ni hatari.

Kumbuka mtu anakuwa kajengea watu wake matumaini ambayo suddenly yanakuja kutoweshwa ghafla. Tell me! Ni wakati wa tume ya Sheria kuanza kuona mchakato wa kurekebisha baadhi ya Sheria za kizamani na ambazo ukweli hazifanyi maisha kuwa realistic na zinakwamisha maendeleo ya watu na nchi kwa maana hiyo. Wasaalamu.
 
Mwenye kujua hizo sifa atuwekee hapa
Ili baada tusijeambiwa walitenguliwa kwa uonevu tuu
 
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Jaji Kaijage amesema uteuzi wa wagombea Urais wa JMT utafanyika tarehe 25/08/2020.

Jaji Kaijage amesisitiza kuwa ni wagombea wenye sifa ndio watakaoteuliwa kuwakilisha vyama vyao kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.

Chanzo: ITV habari!
Yap picha ndo inaanza sasa
 
Kama mdau wa sheria and as far as I remember "Qualifications for election as President" are provided for in Article 39 of the Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 (as amended until 2005).
 
Kwa haya makatazo kibao yanayoendelea nchini kwetu inabidi tu wapinzani mjiandaye kisaikolojia.

Ukweli ni kwamba CCM chama changu hakitaki kuwa na mpinzani October...hivyo nyie kujiondoa na kusema mna imani na mwenyekiti wangu itakuwa jambo la kheri sana
 
Back
Top Bottom