Uchaguzi 2020 Mwenyekiti NEC: Uteuzi wa wagombea Urais utafanyika tarehe 25/08/2020 kwa wale wenye Sifa!

Uchaguzi 2020 Mwenyekiti NEC: Uteuzi wa wagombea Urais utafanyika tarehe 25/08/2020 kwa wale wenye Sifa!

Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Jaji Kaijage amesema uteuzi wa wagombea Urais wa JMT utafanyika tarehe 25/08/2020.

Jaji Kaijage amesisitiza kuwa ni wagombea wenye sifa ndio watakaoteuliwa kuwakilisha vyama vyao kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.

Chanzo: ITV habari!

Nyumbu wa Lumumba mnahamu Lissu afanyiwe Figisu hapa, Amini amini nawaambieni Jiwe ndio hana sifa, NEC watamchinjilia Mbali
 
Nyumbu wa Lumumba mnahamu Lissu afanyiwe Figisu hapa, Amini amini nawaambieni Jiwe ndio hana sifa, NEC watamchinjilia Mbali
Lisu atadhughulikiwa kwenye sanduku la kura bwashee!

Usiogope.
 
ccm ajenda yenu ni kurudi mfumo wa chama kimoja na mlimweka rais huyu ili kukamilisha hayo yite
 
Mfano akimkata, lisu kama lisu atafanyaje?, Ataenda mahakani kulalamika au atakimbilia kwa jirani anakohutubia kila siku au kwa mabeberu?, Au ataitisha maandamano kamw mange?
TATIZO lenu ni mmeshatambua waziwazi kuwa hamumuwezi Lisu.
Kama mafarisayo mtahangaika na kubabaika sana haitawasaidia.
Lissu yupo leo na hata kesho, tutakutana 28/10.
 
Jaji hatma ya Tanzania ipo mikononi mwako...timiza wajibu wako kwa HAKI taifa litakuinua..

Vinginevyo....!! sisi hatutakiwepo huko utakapokuwa unakwenda!!
Ajaribu kulamba sumu aone nini kitamtokea
 
Hapa naona copy&paste ya uchaguzi wa serikali za mitaa
Nami naona hapo ni copy &paste ya hali ya kisiasa ya zamani DRC.
Vijana kuwakuta makundi kama Maimai, FDR, Mbwa kachoka nk itakuwa ndio fasheni.
 
Piga kelele mtandaoni baadae ukalale.
POLE ndugu,
Hutakiwi kujiruhusu kuwa na hasira.
Ukiishamaliza kubwata nenda kanywe maji, maana huruhusiwi kulala.
Kukimbizana na bk7 ni kazi kweli kipindi hiki.
 
Kujipanga kufeli kabla ya mtihani tayari kuna tafsiri nyingi... ila tukumbuke kufaulu ni matokeo ya usikivu, kufata sheria na miongozo pamoja bidii ya muda mrefu, hakuna miujiza hapo
".........Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumtupia jiwe..........." AMEN
 
Kama mtu hana sifa kwanini wakampa fomu?

Kwani inawezekana chizi siku moja akaenda kuchukua fomu ya Urais wakampa?

Huyo jaji aache kuchezea akili za watu, tumeshajua mgombea wetu ni nani na kura zetu anazo, yeye na hayo matamko yake ya ajabu ajabu anajifurahisha tu.
Nahisi watakuwa wanatengeneza mazingira ya sisi kuamini kuwa hawawezi kujua sifa za anaechukua hizo fomu hadi pale atakapozijaza ndiyo watajua hizo sifa za mhusika kupitia maswali watakayokuwa wanamuuliza ndani ya hiyo fomu( kama fomu ina maswali lakini)
 
Alishawambia mapema chukueni tahadhali wakati wa kupitisha wagombea wenu, hakikisheni hawana vizingiti.
Sasa siku mkipewa kizingiti ndo mtachoka.
Ndio tumaini lenu kuu? Mwatia huruma kweli.
 
Back
Top Bottom