Maalim Seif Hamad amesema kuwa Rais Magufuli akizungumza na balozi mwaka huu alimhakikishia balozi kuwa kutakuwa na uchaguzi huru na haki na wazi lakini amesema kwa sasa wananchi wanachokishuhudia ni tofauti kabisa na maneno hayo na si tu kwa Tanzania bara lakini pia hata Zanzibar unga umezidi maji.
Amesema wanayo taarifa Pemba karibu wagombea wote wa ACT-Wazalendo waliwekewa pingamizi za kipumbavu kabisa na kwa sasa 8 kati yao wameruhusiwa kuendelea kugombea na 10 bado wanasubiri maamuzi.
Ambapo jambo la kusikitisha ni kwamba wanaoweka pingamizi ni wasimamizi wa uchaguzi ambao kwa mara ya kwanza Tangu historia ya Zanzibar wametolewa kutoka bara na wote ni maafisa wa usalama wa Taifa wamekuja kwa maagizo maalum ya Rais Magufuli kwa waahakikishe kwamba wagombea wa ACT-Wazalendo wanaenguliwa.
Amesema kuwa unakuta wagombea wanaambiwa wamewekewa pingamizi na mgombea wa chama fulani na wakati huohuo mwanachama huyo anakataa kuwa hajaweka pingamizi anakataa mwenyewe anasema si kweli kwamba hajaweka pingamizi kwa barua.