Zanzibar 2020 Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif atoa msimamo juu ya wagombea ACT-Wazalendo kuenguliwa

Zanzibar 2020 Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif atoa msimamo juu ya wagombea ACT-Wazalendo kuenguliwa

Wewe bado mtoto pengine huu ni uchaguz wako wa pili kushuhudia

Znz iko hivyo siku zote lakin mwishowe mpira unaokotwa nyavuni baadae October
Sasa uchaguzi wa nini. Mnalo safari hii
 
Magufuri atamwaga damu mwaka huu, ujio wa lissu umemchanganya, yuko tayari kung'ang'ania madaraka kwa namna yoyote ile.
asije kutuletea aibu ya majeshi ya east africa kuja hapa eti kulinda amani.

hatutaki yatokee yaliyotokea Gambia, ajiandae rasmi kukukubali maamuzi yetu kama anavyoyategemea, huu ujanja ujanja anaotaka kufanya ili uchaguzi usifanyike hautamfanya aendelee kuwa rais.

uchaguzi ni lazima ufanyike ili aondoke.
Shetani hawezi kuondoka mwenyewe au kwa majadiliano. Shetani huondolewa. Amen
 
Watu waliomzunguka Pombe wamejaza sifa kwenye mashavu kuliko ushauri
 
Huu utawala wa bwana Pombe utaipeleka hii nchi Pabaya sana
 


Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, ametowa msimamo wake juu ya hatua ya wasimamizi wa uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwaenguwa wagombea ubunge wa chama chake maeneo mbalimbali.

Msikilize hapa

 


========

Maalim Seif Hamad amesema kuwa Rais Magufuli akizungumza na balozi mwaka huu alimhakikishia balozi kuwa kutakuwa na uchaguzi huru na haki na wazi lakini amesema kwa sasa wananchi wanachokishuhudia ni tofauti kabisa na maneno hayo na si tu kwa Tanzania bara lakini pia hata Zanzibar unga umezidi maji .

Amesema wanayo taarifa Pemba karibu wagombea wote wa ACT waliwekewa pingamizi za kipumbavu kabisa na kwa sasa 8 kati yao wameruhusiwa kuendelea kugombea na 10 bado wanasubiri maamuzi.

Ambapo jambo la kusikitisha ni kwamba wanaoweka pingamizi ni wasimamizi wa uchaguzi ambao kwa mara ya kwanza Tangu historia ya Zanzibar wametolewa kutoka bara na wote ni maafisa wa usalama wa Taifa wamekuja kwa maagizo maalum ya Rais Magufuli kwa waahakikishe kwamba wagombea wa ACT wanaenguliwa.

Amesema kuwa unakuta wagombea wanaambiwa wamewekewa pingamizi na mgombea wa chama fulani na wakati huohuo mwanachama huyo anakataa kuwa hajaweka pingamizi anakataa mwenyewe anasema si kweli kwamba hajaweka pingamizi kwa barua .
Nimependa kauli ya Maalim liwalo na liwe
 
Kuna video inazunguka Mwanyekiti wa ACT wazalendo bwana Seif anasema Sasa inatosha.

Inakuwaje watu kutoka bala wapelekwe Zanzibar kusimamia uchaguzi?

Inakuwaje waje na maelekezo kutoka juu? Kwa Magufuli?

Inakuwaje wawe maafisa wa usalama wa taifa?

Inakuwaje vyama vingine vilazimishwe kuwawekea pingamizi wagombea wa ACT?

Amesema Sasa basi inatosha.
View attachment 1550611View attachment 1550612
hata akisema hivyo inatosha atafanyaje sasa anahamasisha watu wafanye fujo wakamatwe ? atangulie yeye na familiayake
 
NEC na wanaopanga hiyo mipango ya hujuma wajitafakari, hao watu wameoleana na wengine ni ndugu hivyo mipango mibaya inayopangwa lazima wataambiana tu hivyo anayekuwa amepanga lazima atachukiwa.
 
Wewe si ulikwenda ikulu ukatoka unakenuwa meno ukatwambia kakuhakikishia uchaguzi utakuwa huru na wa haki? Ulikosea sana kuwazuwia wanachama wako 2010 na 2015. What a missed opportunity it was!
Kwani na hawo walioachiwa wamefamya nini chá maana?
 
Inasemekana hao jamaa wa tume tayari wameshajuulikana wanapoishi na mienendo yao yote, vijana wamejipanga kuhakikisha hawarudi kwao wakiwa wazima. Linangojewa tamko tu. Kuweni makini vyombo vya usalama, musisubiri watu wafe ndio mnaenda kufanya uchunguzi.
 
Kama CCM haitaki kuondoka kwa kura za kidemokrasia basi wanataka kuondolewa kwa risasi.
 
Muangalie Maliim body language yake na hasa macho yake halafu ulinganishe na kile anachosema. Najiuliza tumefikaje hapa? NEC isipochukua hatua kitanuka jamani. Je ni lazima tufike huko? Tafakari tunaipeleka wapi nchi yetu. Mola atusaidie-baada ya Jecha ndio hili balaa, wanaosikia wasikie vinginevyo,,,,,,
Kwa age yake Kuna uwezekano mkubwa hii ikawa term yake ya mwisho na hicho ndicho kinachomvuruga zaid
 
Back
Top Bottom