Zanzibar 2020 Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif atoa msimamo juu ya wagombea ACT-Wazalendo kuenguliwa

Wajumbe

Senior Member
Joined
Jul 26, 2020
Posts
136
Reaction score
379
Your browser is not able to display this video.

Maalim Seif Hamad amesema kuwa Rais Magufuli akizungumza na balozi mwaka huu alimhakikishia balozi kuwa kutakuwa na uchaguzi huru na haki na wazi lakini amesema kwa sasa wananchi wanachokishuhudia ni tofauti kabisa na maneno hayo na si tu kwa Tanzania bara lakini pia hata Zanzibar unga umezidi maji.

Amesema wanayo taarifa Pemba karibu wagombea wote wa ACT-Wazalendo waliwekewa pingamizi za kipumbavu kabisa na kwa sasa 8 kati yao wameruhusiwa kuendelea kugombea na 10 bado wanasubiri maamuzi.

Ambapo jambo la kusikitisha ni kwamba wanaoweka pingamizi ni wasimamizi wa uchaguzi ambao kwa mara ya kwanza Tangu historia ya Zanzibar wametolewa kutoka bara na wote ni maafisa wa usalama wa Taifa wamekuja kwa maagizo maalum ya Rais Magufuli kwa waahakikishe kwamba wagombea wa ACT-Wazalendo wanaenguliwa.

Amesema kuwa unakuta wagombea wanaambiwa wamewekewa pingamizi na mgombea wa chama fulani na wakati huohuo mwanachama huyo anakataa kuwa hajaweka pingamizi anakataa mwenyewe anasema si kweli kwamba hajaweka pingamizi kwa barua.
 
Kuna video inazunguka Mwanyekiti wa ACT wazalendo bwana Seif anasema Sasa inatosha.

Inakuwaje watu kutoka bala wapelekwe Zanzibar kusimamia uchaguzi?

Inakuwaje waje na maelekezo kutoka juu? Kwa Magufuli?

Inakuwaje wawe maafisa wa usalama wa taifa?

Inakuwaje vyama vingine vilazimishwe kuwawekea pingamizi wagombea wa ACT?

Amesema Sasa basi inatosha.
View attachment 1550611View attachment 1550612
 
Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, ametowa msimamo wake juu ya hatua ya wasimamizi wa uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwaenguwa wagombea ubunge wa chama chake maeneo mbalimbali.

Msikilize hapa

 
Tumefika huku?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…