Mwenyekiti wa Barazaa la Makanisa ya Kipenteksote Mkoa wa Dar es Salaam, Mchungaji Emmanuel Mwasota amesema tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu 2025 lipo kwa ajili ya maombi ya kuombea uchaguzi huo.
Mchungaji Mwasota amewataka waumini wa madhehebu yote nchini kuiombea nchi ya Tanzania, viongozi wake, wabunge, madiwani na rais ili uchaguzi uweze kupita kwa amani.
"Sisi tunasema kwamba tutashikana kwa pamoja na taarifa hizi zinaenda kila mahali kwa makanisa, wachungaji, maaskofu na wahubiri wa aina mbalimbali tutakuwa pamoja kwa ajili ya kuhakikisha tunaombea nchi yetu ipite salama kwenye uchaguzi utakaofanyika mwaka huu," alisema Mchungaji Mwasota.
Mwasota aliongeza kuwa, uchaguzi unaweza kusababisha nchi kupasuka kama raia wake wasipokuwa wazalendo, hasa kwa upande wa amani kwa ajili ya kuombea nchi na viongozi wake.
Alisema ni muhimu kuombea uchaguzi na viongozi watakaochaguliwa ili waongoze nchi.
Wakati huohuo, wadau mbalimbali na Watanzania wameombwa kujitokeza kwa wingi kudhamini Tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu litakalofanyika katika mikoa 26 nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 2, 2025, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama amesema tamasha hilo halitakuwa na kiingilio ili kila Mtanzania aweze kushiriki kwenye kuliombea taifa huku maandilizi yakiwa yanaendelea vizuri.
Msama ameongeza kuwa, tamasha hilo litaanzia Dar es Salaam na kwenda mikoa mingne na limehusisha wachungaji, maskofu wa mikoa mbalimbali katika kuhakikisha wanaombea amani kulekea Uchaguzi Mkuu 2025.
Aidha, Msama amesema waimba Injili mbalimbali wakubwa kutoka nchini na nje watakuwepo kwenye tamasha hilo la aina yake.
"Tutatangaza tarehe na eneo ambalo tamasha hilo litafanyika hivi karibuni kwa Mkoa wa Dar es Salaam," amesena Masama.