Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CHADEMA, Mkoa wa Mbeya asema CHADEMA imejaa watu wenye roho mbaya, asema uchaguzi wa chama umejaa rushwa ya kutisha

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Ukiona moshi, usidhani uko Mkoa wa Kilimanjaro, wakati mwingine ni moto unawaka chini kwa chini.

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Chadema Mkoa wa Mbeya amekiri kwamba uchaguzi ndani ya chama umejaa rushwa ya kiwango cha kutisha, kiasi kwamba aliamua ajiondoe kuogombea uenyekiti wa chama mkoa wa Mbeya.

Ameendelea kusema kwamba chama hicho kimejaa watu wenye roho mbaya sana kuliko hata CCM.

Full video, tembelea youtube page ya Jambo.

 
I say, hasira ya kushindwa uchaguzi mbaya sana, hata kama uchaguzi ulikuwa wa haki. Aliyeshindwa ataongea lolote lile. Ni aina ya hasira ya kuvunja mapenzi na mwanamke wakati bado anakupenda (a woman scorned). Utazushiwa kila kitu - kibamia, unajamba ovyo, huridhishi, mshamba nk!
 
Hata Putin kashinda tena, unafikiri ni mapenzi ya watu kuwa wanampenda saaaanaaa
 
Chama kusemana na kukosoana ni jambo la afya sana. Nawashukuru Chadema wana uhuru wa kutoa mawazo na kusema. Lakini sisi kijani ni zidumu fikira za Mkiti tu hata kama hafanyi vizuri
 
Na ni fomu moja tu sasa ole wako utie pua
Halafu unakuta sisi ambao hatuna uhuru wa kujieleza ndio tunawasema vibaya Chadema. Kwa kweli kuwa CCM ni sawa na jera ila kwa vile tuko ili tupige diri tu na ni chama cha wapiga diri tunaendelea kukomaa humo humo na diri zetu.
 
Demokrasia ya kuzungumza ndani ya Chadema ni kubwa mno
 
Hicho ni chama Cha waganga njaa wako kimaslahi ndio maana wanataka kutoana roho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…