Mwenyekiti wa Bodi: Simba tumejipanga kusajili wachezaji wenye njaa ya mafanikio

Mwenyekiti wa Bodi: Simba tumejipanga kusajili wachezaji wenye njaa ya mafanikio

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, Salim Abdallah 'Try Again' amezungumza na Azam Tv kwamba, rais wa heshima wa timu hiyo Mohammed Dewji 'MO' anarudi kusajili.

Try Again amesema kuwa tayari wamefanya kikao na rais wa heshima wa Simba SC, Mohammed Dewji'MO' watasajili kwa kishindo ili msimu ujao wafanye maajabu.

"Tumeshindwa kufanya vizuri msimu huu hilo halitutoi mchezoni, tumekutana kama viongozi kwa lengo la kusawazisha makosa yetu hilo limefanyika kwa usahihi".

"Tutasajili wachezaji ambao wana njaa ya mafanikio, tutabaki na wachezaji kadhaa, kuna wengine mikataba yao imekwisha, na wengine kutokana na viwango vyao tutawaaga, lakini nawapongeza wachezaji wetu wamepambana kweli kweli".

"Na kwa sasa tunafanya mchakato wa kupitia CV ya makocha waliotuma maombi na baada ya kumpata atakayekuwa sahihi kabla ya msimu huu haujaisha atapewa nafasi ya kutoa mapendekezo ya usajili na tutaanza bila kuchelewa ili tuendane na mbio za maandalizi mazuri ya mwanzo wa msimu 'Pre Season".
amesema Try Again

Wakati huo huo Try Again alitaja sababu zilizomuondoa Kocha Pablo Franco Martin kuwa ni kushindwa kufikia malengo ya klabu, kutwaa taji la Ligi Kuu, Kombe la Azam Sports Federation Cup, Klabu Bingwa Afrika hatua ya Nusu Fainali, ambayo yalikuwa kama sehemu ya makubaliano ndani ya mkataba.
HUO USAJILI WENYEWE SASA!
 
Duh, ni Timu yote sasa..! Ila kwa Matola haiwezekani kuendelea kubakia hapo Simba, na njia ya kumuondoa ni Kocha mpya kuja kuchagua msaidizi wake mwenyewe..!

Banda na Kanoute waendelee, bado wana nafasi ya kuonyesha uwezo wao

Halafu mbona Gadiel na Dilunga hawapo?
Banda tuwe wakweli yule anatumalizia pesa
Simba si timu ya kukuza vipaji, twatakiwa kushinda, hatupaswi vumilia watu.
Banda apelekwe mkopo akapate playtime yakutosha
 
Majinga San nyinyi mnaenda kuwatafuta wachezaji nnnje na kuwalipa mamilion of dollars acheni upuuz Simba itatwaa taji la caf ma shirikisho endapo tu watakuwa na wachezaji watano wa kigeni wenye hadhi ya juu sna
 
Mmiliki akishasema, hakuna wa kumpinga! Mnachotakiwa mashabiki kwa sasa ni kujiandaa tu kumsifia mitandaoni kwa usajili atakao ufanya msimu.

Halafu suala la bilioni 20, achana nalo! Litakuletea matatizo. Huna sababu ya kuhoji wakati timu imefika robo fainali klabu bingwa Afrika na shirikisho mara kadhaa, ndani ya miaka michache!

Nani kama Dr. Moo na Try Again,
[emoji2788] Hakunaaaa!!!!
Tate mkuu , unafikiri Yanga wasipomsifia giesiemu Yanga haitashuka daraja? Au umesahau kipindi kile cha changia Yanga isitelemke daraja? Kwa hawa matajiri wakati mwingine lazima ukubali kujishusha ilimradi tu mambo yako yaende sawa.

Kule Yanga ulishasikia mtu anaemhoji GSM kuhusu mauzo ya jezi? Watu wanajua jinsi jamaa anavyokunja mpunga wa Kufa mtu kutokana na mauzo ya jezi lakini hawasemi .Siku mkihoji tu GSM anasepa na timu inashuka daraja.

Itoshe tu kusema kuwa bila hawa matajiri mpira wa bongo utarudi kule tulikotoka miaka 25 bila kuona klabu ya Tz ikiingia angalau hata hatua ya makundi ktk mashindano ya CAF
 
Mbona kabla ya huyo GSM Yanga ilijiendesha pasipo mdhamini! Na bado timu ilifanya vizuri wakati kocha akiwa ni Mwinyi Zahera! Hawa Wahindi ni wezi tu siku zote.
 
Kiuhalisia, si rahisi kutengeneza timu yoyote ile ikafikia nusu fainali ya mashindano ya vilabu vya Bara lolote lile kwa kuanza na wachezaji wapya wengi kuliko waliobakishwa. Huo unakuwa ni Mradi mpya unaohitaji zaidi ya mwaka mmoja kukamilika.
msimu huu waliuzwa wachezaji wawili tu ,waliobaki wote ni wale walikuwepo misimu iliyopita,mbona hawakuingia nusu fainali?
 
Kama kweli tunataka kuvuka pale tunapoishia yaani robo fainali na kwenda mbele nusu au fainali ya michuano ya CAF, bila shaka wachezaji hawa pamoja na Kocha msaidizi Matola tungewaaga, kwa kuwashukuru.

Mhilu (mkopo)
Jimmyson (mkopo)
Gadiel
Nyoni
Dilunga
Mzamiru
Mugalu
Kagere
Wawa
Lwanga
Bwalya
Morrison
Dilunga mpe heshima yake,huyo ni mtu na nusu. Kua majeruhi kusikufanye usahau mchango wake kwenye timu. Ni mmoja kati ya wachezaji wazawa ambao akiwa fit lazima acheze toka enzi za Patrick Aussems. Bila kumsahau Mzamiru, namaanisha Dilunga na Mzamiru watoe kwenye hilo kundi.
 
Utakuwa chizi wa takwimu...simba ya mwaka huu ni sawa na mtu aliyesoma sana na hana hela yaani choka mbaya. Anaishia kujisifu alivyo na madegree huku anabangaiza maisha. Unajitapa uko namba 12 caf huku huna kombe lolote LA maana.
Hahaaaa.....kichekesho cha mwaka mna mpaka Rais wa heshima. Yaani kilakitu ni cha kufikirika tuu.
Mikia buuaana!
 
Kama vipi hata Chama ikiwezekana asepe tu,lipite fagio la chuma hasa.
 
shida si kusajili bali kuwatumia kwa usahihi wachezaji waliosajiliwa! hata mwaka huu usajili wenu Mikia FC ulikuwa mzuri sana ila kilichokosekana ni muunganiko wa wachezaji kucheza kitimu, consistently na kwa nidhamu na morali!!

Si vibaya mkimuomba ushauri na mbinu Professor Nabi nyie ni watani zetu sio maadui.

Wachazaji kama Sakho, Kibu, Banda, Inonga na Kanoute ni wazuri mno ila timu yenu haikujenga formation ya kuwaunganisha. Sisi wananchi tunapenda kuipiga timu bora ya Makolo FC sio timu mbovu kama ile mliyoleta CCM Kirumba, mtoto mdogo Feisaaaaaal anatoka na mpira toka katikati ya uwanja na kwenda kumsalimia Kakolanya bila bugudha yoyote!
Hivi unajua Simba ndiyo walifukuzisha kazi Nabi kule Sudan?
 
Hivi unajua Simba ndiyo walifukuzisha kazi Nabi kule Sudan?
kocha huwa mzuri wachezaji wakicheza kwenye plan, Yanga wanacheza kwa plan ya Nabi na Kaze ndo maana hawafungiki. Wachezaji wakicheza wanavyojua wao hata uwe kocha mzuri utafeli kama ilivyotokea kwa Pablo

Kibu anacheza vizuri sana anapunguza wawili Kibwana na Moloko badala ya kutoa pasi anataka eti akapasue na ukuta wa Mwamnyeto na Job kabla hajawafikia hao visiki Feisal anamkatizia kwa mbele na kuchukua boli!

Sakho anachukua mpira kwa kasi anawahadaa na kuwapita Aucho na Sureboy badala ya kutoa pasi anataka akapite katikati ya Mwamnyeto na Job, Kibwana anamkatizia na kubeba boli.

Simba hii hawachezi kitimu
 
Mmiliki akishasema, hakuna wa kumpinga! Mnachotakiwa mashabiki kwa sasa ni kujiandaa tu kumsifia mitandaoni kwa usajili atakao ufanya msimu.

Halafu suala la bilioni 20, achana nalo! Litakuletea matatizo. Huna sababu ya kuhoji wakati timu imefika robo fainali klabu bingwa Afrika na shirikisho mara kadhaa, ndani ya miaka michache!

Nani kama Dr. Moo na Try Again,
[emoji2788] Hakunaaaa!!!!
Kwani nyie hapo utopoloni kuna wa kumbishia Ghalib? Nyie watu wa kumchekea Haji Manara? Nyie ni wa kumpokea Kwa shangwe Morrison? Siku zote anayemlipa mpiga zumari ndiye anachagua nyimbo, chukua hiyo mkuu!!
 
kocha huwa mzuri wachezaji wakicheza kwenye plan, Yanga wanacheza kwa plan ya Nabi na Kaze ndo maana hawafungiki. Wachezaji wakicheza wanavyojua wao hata uwe kocha mzuri utafeli kama ilivyotokea kwa Pablo
Ukweli japo unauma lakini lazima usemwe,Simba msimu huu haikuwa na timu nzuri,hata kumfukuza kocha ni kumuonea tu. Mastraika waliofunga magoli zaidi ya arobaini msimu uliopita hadi leo wote watatu hawajafikisha hata magoli kumi Kwa ujumla wao. Asitafutwe mchawi kikosi kilikuwa kimechoka.
 
Ila bongo hatupendani wenyewe na hii shida inaota mizizi kizazi hadi kizazi. Matola aondoke simba kwa sababu gani? Kocha msaidizi anamsaidia kocha mkuu katika kutekeleza falsafa za kocha mkuu. Matola akiwa kocha msaidizi ameipatia simba mataji mangapi?

Matola akiwa msaidizi simba imejitahidi katika anga la kimataifa, ingekua ni busara kumpeleka shule akapate cheti cha juu, ili aje kuisadia timu baadaye kama kocha mkuu au mkurugenzi wa ufundi.

Zinedine zidane alikua msaidizi wa Mourinho pale madridi, baadaya akaja Ancelotti bado akawa msaidizi, alikuja Benitez bado akawa msaidizi. Baadaye timu ikamuamini na kumpa mikoba ya ukocha mkuu, the rest was history. Three times consecutively champions league winner, mpaka anaondoka ni bingwa wa ligi na UEFA.

Sasa waganga njaa mmekazana matola aondoke aondoke hata ubinadamu hamna... jamaa ametoka mbali na timu. Msomesheni na apewe nafasi.
 
Ukweli japo unauma lakini lazima usemwe,Simba msimu huu haikuwa na timu nzuri,hata kumfukuza kocha ni kumuonea tu. Mastraika waliofunga magoli zaidi ya arobaini msimu uliopita hadi leo wote watatu hawajafikisha hata magoli kumi Kwa ujumla wao. Asitafutwe mchawi kikosi kilikuwa kimechoka.
Bocco amefunga 3 Kagere 7 jumla 10. Sema msimu huu hawajafika 20 kwa hiyo 10 ulosema haihakisi uhalisia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba ya msimu ujao kama sio nusu fainali basi fainali yenyewe
Hata msimu huu maneno yalikuq hayo hayo mkaja kubadili gear angani GSM ananunua match,now mmechange tena gear mtasajili wachezaji wenye njaa,timu la magazeti
 
Attachments

  • 20220521_002908.jpg
    20220521_002908.jpg
    136.2 KB · Views: 9
Back
Top Bottom