LGE2024 Mwenyekiti wa CCM Simiyu, Shemsa Mohamed asisitiza wajibu wa kila Mwanachama kwenye ushindi wa CCM

LGE2024 Mwenyekiti wa CCM Simiyu, Shemsa Mohamed asisitiza wajibu wa kila Mwanachama kwenye ushindi wa CCM

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Political Jurist

Senior Member
Joined
Sep 6, 2021
Posts
143
Reaction score
120
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Ndg. Shemsa Mohamed, ameendelea na kampeni yake ya kutafuta kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, akizungumza na wananchi na vijana wa UVCCM katika Wilaya ya Bariadi. Katika kampeni hiyo, alisisitiza umuhimu wa vijana kushiriki kikamilifu katika kutafuta kura za Wenyeviti wa Mtaa, Vijiji, na Vitongoji wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi, ili kuhakikisha ushindi mkubwa katika uchaguzi ujao utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024.

Ndg. Shemsa aliwaambia vijana wa UvCCM kuwa wao ni nguzo muhimu katika kuhakikisha ushindi wa chama, na akawataka kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha umma na kutoa mwamko kwa wananchi wa maeneo yao. Aliwakumbusha kuwa ushindi huu hautaongeza tu nguvu ya chama bali pia utasaidia kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi wote.

"Chama chetu kina imani kubwa na vijana, nanyi ni sehemu muhimu ya mabadiliko na mafanikio ya kitaifa. Kwa kushirikiana, tutapata ushindi mkubwa na kuweka historia ya mabadiliko kwa wananchi wa Simiyu," alisisitiza Mwenyekiti Shemsa.

Baada ya ziara hiyo, Mwenyekiti aliendelea na kampeni hiyo katika Wilaya ya Meatu ambapo alikutana na wananchi, Wana CCM, na wagombea wa nafasi mbalimbali. Katika kikao cha ndani, Mwenyekiti Shemsa Mohamed aliwaeleza Wana CCM kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni fursa muhimu kwa kila mwanachama kufanya kazi kwa umoja ili kushinda kwa kishindo. Alisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano na kushirikiana na wagombea katika kufanya kampeni, kuwafikia wananchi kwa karibu, na kutatua changamoto zinazowakabili.

"Kamwe tusikubali kupuuzilia mbali nafasi ya kila mmoja wetu ndani ya CCM. Ushindi wetu unategemea kazi ya kila mmoja wenu. Hivyo, lazima tuonyeshe umoja, kujitolea, na kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kwamba tunaendelea kuwa chama kinacholeta maendeleo kwa wananchi," alisema Mwenyekiti Shemsa katika kikao hicho cha ndani.

Aidha, Mwenyekiti alikumbusha Wana CCM kuwa uchaguzi huu sio tu suala la ushindi bali ni hatua muhimu katika kuendelea kuleta mageuzi chanya kwa wananchi wa Meatu na Simiyu kwa ujumla. Alitoa wito kwa kila mwanachama kuhakikisha kuwa anahamasisha jamii zote za wilaya hiyo kwa kuwatembelea na kueleza faida za kuwa na viongozi wa CCM, wakiwa na dhamira ya kuwatumikia wananchi.

Imetolewa na Idara ya Siasa na Uenezi Mkoa wa Simiyu
IMG-20241124-WA0077(1).jpg
IMG-20241124-WA0074(1).jpg
 
Ccm haiwezi kushinda kupitia sanduku la kura,kwanza wanashindanishwa na nani?
 
Back
Top Bottom