MPANDA Jr
JF-Expert Member
- Nov 27, 2011
- 1,295
- 159
Mwenyekiti wa CCM Wilaya mpya ya Gairo Bwana Omary Awadhi, amemwagiwa tindikali usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Gairo. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo tukio hilo lilitokea usiku wa manane baada ya watu wasiojulikana kumgongea na kumwamsha.
Hata hivyo anasema aligoma kufungua mlango bali alifungua kioo cha dirisha la chumbani kwake. Watu hao walimuonya kutohudhuria kikao ambacho yeye ni mhusika alipokataa, ndipo ghafla akahisi kumwagiwa kitu usoni kilichomletea maumivu makali sana.
Aliwahi kunawa maji lakini hali bado ni tete.Muda huu yupo safarini anakimbizwa Dar kwa matibabu zaidi baada ya uso wake kuharibika.
GAIRO
---------------------------------------
- Uelewa wangu juu ya kundi la watu wasiojulikana
~ Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

PIA SOMATaarifa toka kwa mjumbe wa Jumuiya ya Wazazi (Jina kapuni) anasema kumekuwepo mvutano wa muda mrefu kati ya Mwenyekiti huyo na Mbunge wa jimbo hilo la Gairo Mhe: Ahmed Shabiby. Mgogoro huo ulichukua sura mpya baada ya ziara ya Kinana kwani mwenyekiti alimtuhumu Mbunge huyo kugawa chama huku na yeye akitangaza kugombea ubunge 2015. Kikao kilichosababisha mtafaruku huo ni cha tarehe06/07/2013 kuhusu wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na Mwenyekiti huyo ambaye magaidi waliomdhuru walimtaka asihudhurie.