Mwenyekiti wa CCM Wilaya mpya ya Gairo Bwana Omary Awadhi, amemwagiwa tindikali usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Gairo. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo tukio hilo lilitokea usiku wa manane baada ya watu wasiojulikana kumgongea na kumwamsha.
Hata hivyo anasema aligoma kufungua mlango bali alifungua kioo cha dirisha la chumbani kwake. Watu hao walimuonya kutohudhuria kikao ambacho yeye ni mhusika alipokataa, ndipo ghafla akahisi kumwagiwa kitu usoni kilichomletea maumivu makali sana.
Aliwahi kunawa maji lakini hali bado ni tete.Muda huu yupo safarini anakimbizwa Dar kwa matibabu zaidi baada ya uso wake kuharibika.
GAIRO
---------------------------------------