Ngoja tuangalie list ya waliwahi kupatwa na dhahama ya kufanyiwa kitu kibaya ili tujue ni CDM au la.
- Horace Kolimba aliitwa Dodoma kwenye kikao cha ccm ili wamuulize ni kwanini kasema ccm imepoteza Dira? alipoingia kikaoni, hakurudi tena, bila shaka watakua CDM waliofanya vile.
- Imrani Kombe (rafiki wa karibu na Augostine Lyatonga Mrema) mara baada ya kuvujisha siri ya msamaha wa kodi na mrungura wa Tsh 900M kwa kigogo wa ccm aliopewa na wafanya biashara wa mafuta na viwanda vya samaki kule Mwanza, alipigwa risasi na polisi, nadhani hi nayo ilikua ni CHADEMA hawa.
- Kijana alikuwa dereva wa gari lililomuua marehem Chacha Wangwe (MP, RIP) alikutwa hana leseni ya udereva, pamoja na kwamba alisababisha ajali ilichukua uhai wa Mbunge, rais alimuachia kwamsamaha wa raisi na sasa yupo mtaani, hili nalo nadhani ni CDM.
- Yasemekana mwalimu Nyerere alikataa kwenda kutibiwa UK (Nimeitoa hii siri kwenye kampeni za Ubunge pale USA river, by campegn manager wa CDM) na Mkapa akalazimisha, Nyerere hakurudi hadi leo, mara baada ya kifo chake, kulitokea ufisadi wa kutisha, nahisi hata hiki kifo ni kilipangwa na CHADEMA.
- Kifo cha marehem Daudi Mwangosi akiwa chini ya mikono salama ya polisi tena kwa ulinzi madhubuti wa RPC wa Iringa, alipigwa bomu na mwili wake kusambaratishwa, RPC sasa kapandishwa cheo, hili nalo akili yangu inanituma kua ni CDM.
- Kibanda, Ulimboka n.k, nao sijui ni CDM? mbona sasa waziri alilifungia gazeti la Mwanahalisi wakati lilitoa full story ya mteseji wa Dr. Uli? CHADEMA bwana!
- ....
- n.k
Sijui kama bado tutasema ni CHADEMA kweli, lakini pia, kama ni CDM wanafanya haya, inakuaje usalama wa taifa uwe kimya na hata washinikize wauaji wapndishwe vyeo?