Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo amwagiwa Tindikali na watu wasiojulikana

MPANDA Jr

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2011
Posts
1,295
Reaction score
159
Mwenyekiti wa CCM Wilaya mpya ya Gairo Bwana Omary Awadhi, amemwagiwa tindikali usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Gairo. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo tukio hilo lilitokea usiku wa manane baada ya watu wasiojulikana kumgongea na kumwamsha.

Hata hivyo anasema aligoma kufungua mlango bali alifungua kioo cha dirisha la chumbani kwake. Watu hao walimuonya kutohudhuria kikao ambacho yeye ni mhusika alipokataa, ndipo ghafla akahisi kumwagiwa kitu usoni kilichomletea maumivu makali sana.

Aliwahi kunawa maji lakini hali bado ni tete.Muda huu yupo safarini anakimbizwa Dar kwa matibabu zaidi baada ya uso wake kuharibika.

GAIRO

---------------------------------------

PIA SOMA
- Uelewa wangu juu ya kundi la watu wasiojulikana

~ Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia

- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
 
Na hao ni CDM?? mmeparanganyika na hata hamuwezi kurudi kuwa wamoja tena kwa laana ya kuua na kuibia watanzania.
 
CCM mnaanza kujidhiilisha kuwa nyie ndo wamwaga tindikali. Duh ashukuliwe Mungu. Ukweli utazidi kudhiilika.
 

kwenye red hao watakuwa wana ccm wenzake,kugombeana vyeo na pesa
 

Mleta mada inaonekana kuna kitu unajaribu kukificha sijui kwa makusudi ama hujui waambie wana JF nikikao gani emwagiwa tindikali alipaswa kuhuzuria, je hao watu waliomgongea mpaka akafungua dirisha hajawajua hata kwa sauti...
 
dhambi ya unafiki haiwaachi huru itawatafuna mpaka mtuombe radhi watanzania!
 
hivi chadema mnaipeleka wapi nchi?? kwann hamuachi kula nyama za watu???
 
kwahiyo Chadema mmejihalalishia staili ya tindikali kwa kwenda mbele
 
Since wanatafutwa viongozi wa cdm na baadhi bado wako dodoma,hatukawii kusikia kuwa mh fulani kakamatwa na kuhusishwa na tuhuma hizi..........
 

Mtajuta kumchagua MWINGULU KUA NAIBU KATIBU MKUU KAZI KWENU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…