Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe. Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Mhe. John Pambalu wamekamatwa na Polisi muda huu uwanja wa ndege Songwe wakijiandaa kuelekea Mbeya, Ukamataji huu umeongozwa na RPC wa Mbeya.
========================
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema anasema “Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu tangu akamatwe (jana Agosti 11, 2024) hatujui yuko wapi, Polisi hawasemi, hatujui kama yeye na wenzake wamekula au la, pia Lissu ana dawa anazotumia kila siku kutokana na majeraha ya risasi na sijui kama amekunywa dawa.”
Ameongeza “Kutokana na hali hiyo, Mbowe alilazimika kusafiri kwenda Mbeya kukutana na Polisi, alipowasili Saa 4 Asubuhi akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana, John Pambalu, Polisi wakawakamata na hatujui wako wapi.”
Pia soma: Uzi Maalum wa Matukio ya Kiusalama kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa, SACP Benjamin Kuzaga simu yake ilipokelewa na msaidizi wake aliyesema “RPC yupo kwenye kikao”
Pia soma=> Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa