Walikata rufaa Mahakama Kuu wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana.
Walifutiwa dhamana hiyo na aliyekuwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri Novemba 23, 2018. Kufuatia uamuzi huo, Mbowe na Matiko, walikata rufaa Mahakama Kuu siku hiyo hiyo, wakipinga kufutiwa dhamana yao chini ya hati ya dharura. DPP aliweka pingamizi la awali akiiomba mahakama hiyo isiisikilize rufaa hiyo pamoja na mambo mengine akidai kuwa haina mamlaka kwa kuwa rufaa hiyo ilikuwa inakiuka matakwa ya sheria
Mbowe na matiko walikata rufaa Mahakama ya Rufaa, na Tarehe 1 Machi Mahakama ya Rufani ilitupilia mbali hoja za rufaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na kuelekeza jalada la rufaa hilo lirejeshwe Mahakama Kuu kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji wa rufaa.