TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

Status
Not open for further replies.
Afande mkoa wa Geita kuna tukio la mauaji KTR/IR/1186/2015, lililotokea leo tarehe 14/11/2015 baada ya ALPHONCE S/O MAWAZO, miaka 39, msukuma, mkulima mkazi wa Geita na Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita pia katika uchaguzi mkuu uliopita alikuwa mgombea ubunge jimbo la Busanda, alishambuliwa kwa silaha za jadi na watu wanaosadikiwa kuwa zaidi ya kumi kati yao mmoja ametambuliwa kwa jina moja la MABEGA, wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa CCM.
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa CHADEMA walikuwa na mkutano wao wa ndani katika mtaa wa Ludete A kata ya Ludete katika mji mdogo wa Katoro na CCM pia walikuwa na mkutano na ndani katika ofisi ya CCM, mtaa wa Njiapanda kata ya Ludete, vyama vyote viwili vilikuwa vinaandaa na kuwaapisha mawakala wao kwa ajili ya uchaguzi wa diwani ambao utafanyika kesho tarehe 15/11/2015 katika kata ya Ludete.

Wakati mkutano wa chadema ukiendelea majira ya 12:35 hrs mwanachama mmoja wa CHADEMA alitoa taarifa kuwa nje ya ukumbi kuna watu wanaosadikiwa kuwa wanachama CCM wanarekodi mkutano wao. Baada ya taarifa hiyo wajumbe wote walitoka nje ya ukumbi wakakutana na kundi la hilo nje ya ukumbi. Watu hao waliwashambulia kwa silaha butu 1. ELIZABERT D/O PASCHAL, miaka 43, msukuma, mkulima wa Katoro ameumia kisogoni 2. BAHATI S/O MICHAEL, miaka 38, mzinza, mkulima mkazi wa Katoro, amejeruhiwa kichwani. Wametibiwa kituo cha afya Katoro, wameruhusiwa na hali zao zinaendelea vizuri. Kutokana tukio hilo wajumbe wote wa CHADEMA walitawanyika.

Marehemu alitoweka katika eneo hilo katika mazingira ambayo hata wenzake wameshindwa kuyaelezea. Muda mfupi alionekana akipigwa katika umbali unaokadiliwa kuwa nusu kilometa kutoka ukumbi ulipokuwa unafanyika mkutano wao na watu kumi walioshuka kwenye gari aina ya Land Cruiser ambayo namba zake bado hazijafahamika. Baada ya tukio hilo gari hilo lilielekea barabara ya Geita mjini.

Majeruhi alifariki majira ya saa16:00 hrs wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya Geita.

Upelelezi wenye kuambatana na msako mkali unaemdelea kuwatafuta watuhumiwa.
 
Tuliposema hivi vikundi ni hatari kwa ustawi wa amani ya nchi mlibeza kuwa ni mtazamo wa kisiasa,Ikitokea tukavurugwa ni makundi hayahaya yatabeba bendera km zile za Maimai,Bokoharam,Isis nk ni wakati sasa tufikirie kuyafuta
 
Hivi watu humu mna dini? Mliona wapi Mungu anapangiwa kazi za kulipiza visasi!? Kama mnataka kulipiza visasi dhidi ya hao mnao wahisi wamefanya hilo tukio basi hukumu hiyo iwe mikononi mwenu na wala msimuhuhusihe Mungu na hatua mtakazo zichukua au zitakazo chukuliwa kwa waliotenda huo ukatili.

Tumuogope Mungu na jina lake lisitajwe kimzaha mzaha.

Wapo wapakwa mafuta wa Mungu ambao wakiomba lolote kwa Mungu hutenda, ila kama sio mpakwa mafuta Mungu neno lake halina madhara yoyote mbele ya Mungu
 
Wote hao waliofanya , hivyo watalipizwa hapahapa kwani Mungu ameona hayo. Shida je waliofanya hivyo watashughulikiwa?
 
Mbona kamanda Chacha Wangwe hakuzikwa kitaifa na chama wakati alikuwa makamu mwenyekiti wa chama. Mpaka leo hata familia yake mmeitelekeza bila msaada wowote. Acheni uhuni huu.

Kuwa Na roho ya utu wewe! Sidhani kama ukatili huu unafurahiwa Na mwanadamu yeyote awe ni wa itikadi gani. Huu ni unyama wa hali ya juu. Siasa zisitufikishe hata kiasi cha kugharimu damu za watanzania wenzetu. Hizi ni siasa tu. Leo upo ccm, kesho Act, baadae Cdm
 
Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Busanda kupitia CHADEMA bwana Alphonce Mawazo afariki dunia leo.

Chanzo cha kifo chake ni kutokana na kipigo kikali kutoka kwa kundi la vijana linalosemekana ni la green guard jana wakati akifanya kampeni kumnadi diwani wake.

Kamanda Mawazo pia ni mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita.

Kamanda Mawazo pia alikuwa ni member wa JamiiForums (Verified Member)

attachment.php
attachment.php

RIP kamanda
 
hizi laana zinachosha tokaDr mvungiDr Ulimboka KibandaMwangosiTukio la SowetoMoses Machali na KiwiaMch.Mtikilahizi laana zote hawa watu wangekuwa vichaa na watoto waokweli sisi tunamwachia Mungu kila kitu
Mnamwachia Mungu yupi ilhali list inaendelea.Kagenzi.Yule mwandishi wa gazeti la Uhuru aliyekula kichapo kutoka Red Brigade ofisi za CDM Makao Makuu.Acheni unafiki.
 
Siku ya mazishi viongoz wa chadema washirik wote!tuiite mawazo day!nilifurah taifa starz kutoka suluhu,wakati mechi ikiendelea nikapata habar nikanywea mpaka mpira unaisha cjashangilia,nashukuru Mungu mashabik nao walinywea baada ya dk.90,tukaungana sote kwenye huzuni.Japo huzun yangu ilikuwa ya kumpoteza kamanda wangu Alphonce Mawazo.RIP kamanda sote tunakuja.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom