TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

Status
Not open for further replies.
...hahaa, nyie vibuyu wa lumumba bana!

Kenge wewe,
Chacha wangwe alikuwa lumumba? Au tunajua mchezo mzima alikuwa shujaa wetu kwetu huku,pongezi kwa kujua mchezo mzima,
Narudi kwa wazo la Uzi huu, utavuna ulichopanda ukiwa duniani,
 
Tunamkumbuka kijana Musa aliyuwawa Igunga,Mbwambo aliyekatwa Shingo Arumeru,waliouwawa na bomu Arusha,na kwenye maandamano Arusha,muuza msgazeti Morogoro na wengineo
Sasa MAWAZO,nani aliwahi kuhukumiwa kwa mauaji haya?
The saga continues
 
Mimi vurumai za kisiasa huwa nazichukia mno.ZiIwe zinafanywa na CCM au UKAWA (CHADEMA, CUF na kadhalika). Bado nina kumbukumbu na kijana yule aliyemwagiwa tindikali kwenye uchaguzi mdogo wa Igunga. Nikimuona machozi huwa yananilengalenga. Kuna yule mwandishi wa UHURU alitekwa wakati akiwa kazini akapigwa na 'mabondia' wa CHADEMA eti kwa kisingizio kuwa alikuwa amekwenda kuipeleleza CHADEMA au kuandaa maandamano feki. Upo wakati mgombea ubunge wa viti maalum wa CHADEMA alimteka mtazamaji wa ndani wa uchaguzi na kumpeleka polisi kwa kisingizo kuwa alkuwa anapeleleza CHADEMA. Huko poiisi akageuza kibao eti alikuwa anamuokoa. Sasa MAWAZO amekufa sababu ya siasa ......inauma sana.
 
Afande mkoa wa Geita:

kuna tukio la mauaji KTR/IR/1186/2015, lililotokea leo tarehe 14/11/2015 baada ya ALPHONCE S/O MAWAZO, miaka 39, msukuma, mkulima mkazi wa Geita na Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita pia katika uchaguzi mkuu uliopita alikuwa mgombea ubunge jimbo la Busanda, alishambuliwa kwa silaha za jadi na watu wanaosadikiwa kuwa zaidi ya kumi kati yao mmoja ametambuliwa kwa jina moja la MABEGA, wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa CCM.
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa CHADEMA walikuwa na mkutano wao wa ndani katika mtaa wa Ludete A kata ya Ludete katika mji mdogo wa Katoro na CCM pia walikuwa na mkutano na ndani katika ofisi ya CCM, mtaa wa Njiapanda kata ya Ludete, vyama vyote viwili vilikuwa vinaandaa na kuwaapisha mawakala wao kwa ajili ya uchaguzi wa diwani ambao utafanyika kesho tarehe 15/11/2015 katika kata ya Ludete.

Wakati mkutano wa chadema ukiendelea majira ya 12:35 hrs mwanachama mmoja wa CHADEMA alitoa taarifa kuwa nje ya ukumbi kuna watu wanaosadikiwa kuwa wanachama CCM wanarekodi mkutano wao. Baada ya taarifa hiyo wajumbe wote walitoka nje ya ukumbi wakakutana na kundi la hilo nje ya ukumbi. Watu hao waliwashambulia kwa silaha butu 1. ELIZABERT D/O PASCHAL, miaka 43, msukuma, mkulima wa Katoro ameumia kisogoni 2. BAHATI S/O MICHAEL, miaka 38, mzinza, mkulima mkazi wa Katoro, amejeruhiwa kichwani. Wametibiwa kituo cha afya Katoro, wameruhusiwa na hali zao zinaendelea vizuri. Kutokana tukio hilo wajumbe wote wa CHADEMA walitawanyika.

Marehemu alitoweka katika eneo hilo katika mazingira ambayo hata wenzake wameshindwa kuyaelezea. Muda mfupi alionekana akipigwa katika umbali unaokadiliwa kuwa nusu kilometa kutoka ukumbi ulipokuwa unafanyika mkutano wao na watu kumi walioshuka kwenye gari aina ya Land Cruiser ambayo namba zake bado hazijafahamika. Baada ya tukio hilo gari hilo lilielekea barabara ya Geita mjini.

Majeruhi alifariki majira ya saa16:00 hrs wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya Geita.

Upelelezi wenye kuambatana na msako mkali unaemdelea kuwatafuta watuhumiwa.
 
toka nchi yetu ijikomboe kutoka kwa wakoloni,tumekuwa tukisema tanzania ni nchi yenye amani,utulivu,haki,upendo..mimi hayo maneno sikubaliani nayo hata kidogo.

uko wapi uhuru wa kuzungumza?uko wapi uhuru wa kuhoji?uko wapi uhuru wa kushiriki au kushirikishwa?iko wapi haki?iko wapi democrasia?uko wapi upendo??..KAMA TU

-tukihoji utawala tunageuzwa kuwa maadui zao
-tukishiriki harakati tunakuwa maadui zao
-tukiunga mkono wapinzani tunageuzwa kuwa maadui zao
-tukidai haki zetu tunageuzwa kuwa maadui zao
-tukiandika habari zinazowagusa tunageuzwa kuwa maadui zao
-tukishinda tunanya'ganywa ushindi
-tukishinda uchaguzi unafutwa.

"iko wapi HAKI ndugu zangu?,iko wapi DEMOCRASIA ndugu zangu?"... hivi hii TANZANIA ni ya nani?????????hivi kuna mwenye hati miliki juu ya nchi hii..???

1.ikoo wapi HAKI juu ya kifo cha DR.MVUNGI aliyekuwa kamishna wa tume ya mabadiliko ya katiba baada ya kuvamiwa kwake kimara na kujeruhiwa na watu wasiojulikana na hatimaye mauti yakamkuta akiwa hospitali.

2.iko wapi HAKI juu ya utekwaji wa DK.ULIMBOKA aliyetekwa na kutolewa meno,kupigwa nondo,kukatwa na mapanga kisa tu kutetea haki za madaktari.

3.iko wapi HAKI juu ya umwagiwaji wa tindi kali kwa mwandishi na mtafiti mahiri SAED KUBENEA?

4.iko wapi HAKI juu ya utekwaji wa KAMANDA MAWAZO na hitimaye kukatwa katwa mapinga na baada ya siku moja akafariki...???

IKO WAPI HAKI,UKO WAPI UHURU,IKO WAPI DEMOCRASIA,UKO WAPI UPENDO NDUGU ZANGU????....KIUKWELI INAUMA SANA BWANA,HII NCHI NI YETU SOTE NA HAKUNA MWENYE HATI MILIKI JUU YA TANZANIA,KWANINI WANATUFANYIA HIVI LAKINIIIIIII???????
 
Habari Watanzania wenzangu,

Nimesikitishwa saana na kifo cha ndugu yetu Alphonce Mawazo lakini nasikitishwa zaidi na uvumi unaosambazwa wahusika ni green guard wa CCM nashindwa kuamini moja kwa moja kutokana na maneno yaliopo hapa baada ya uchaguzi katika jimbo alilogombea Alophonce Mawazo.

Baada ya matokeo kutoka wafuasi wa CHADEMA katika jimbo hilo walishangazwa na matokeo yaliotoka kwamba kamanda Alphonce ameshindwa katika uchaguzi huo hali iliozusha sintofahamu kwa wafuasi wa chama hicho kutokana na kushindwa kwake na kutoonekana katika eneo la jimbo tangu siku ya mwisho ya kupiga kura na kutangazwa kwa matokeo.

Kutokana na kutoonekana kwa ndugu Alphonce Mawazo katika jimbo kulileta sintofahamu kwa wafuasi wa CHADEMA ndipo zilipozuka fununu ndugu Alphonce Mawazo aliuza jimbo kwa chama tawala na kukubali kushindwa kirahisi, hali hiyo ilileta chuki kwa makamanda wa CHADEMA hali iliyosababisha waape kwa miungu yote kuwa atakapoonekana hadharani ama zao ama zake lazima wamdhuru, ikibidi hata kumuua.

Hivyo kutokana na hasira za wapenzi wa chama hicho nashindwa kuamini moja kwa moja upande mmoja tuu wa green guard wanahusika kwani kama kushindwa alikuwa ameshashindwa ubunge na hakua tishio tena kwa chama cha mapinduzi, kwangu mimi naweza sema kama angekua tishio kwa chama cha mapinduzi basi wangemdhuru wakati anatafuta jimbo lakini sio kwa sasa ambapo hakuwa mshindani hivyo napata ukakasi sana kuamini kama kuna nguvu yoyoye kutoka chama cha mapinduzi ilio nyuma ya kifo cha kamanda Alphonce Mawazo, lakini pia naona kuna watu wanataka kugeuza kifo cha kamanda Alphonce Mawazo mtaji wa kisiasa.

Naomba tutafakari pia hawa wapenzi wa CHADEMA walikuwa wakiapa kuwa lazima watamdhuru baada ya kuhongwa hela ili akubali kupoteza jimbo lakini pia tukiwa tunasubiri matamko ya police na uchunguzi wao ni vema tukawa watulivu kusubiri uchunguzi wa polisi maana yapo pia mambo nje ya siasa ambayo yanaweza pelekea mtu kuumizwa hata kuuwawa ikiwemo biashara, ugoni, imani za kishirikina, ujambazi. nk

Hivyo kabla hatujanyanyua vidole kunyoosheana kwa hisia na kupandikiza uhasama wa kisiasa ni vema tukatafakari upya na kusubiri vyombo vya dola kuleta ukweli. Nichukue nafasi hii kuwapa pole wafiwa na wapenzi wake MUNGU ALITOA MUNGU AMETWA JINA LA BWANA

Tusivutane sana tusubiri taarifa kutoka polise ndio yenye hatima na ukweli huo.
Asante sana ndugu, maana chadema mi nimewashangaa kuanzia jana. Tukio hili siyo la CCM, wajiangalie wao chadema. Picha zilipigwa kwa ustadi wa hali ya juu kama za mtikila, na chacha wangwe.
 
Tuwekee video tuthibitishe maneno yako ----- wewe. Ni lini polisi wako upande wa wapinzani wakafanya uchunguzi na kutoa Ripoti? Au umesahau Mvungi? Umesahau ya Ulimboka? Umesahau maigizo ya jeshi la CCM mlipuko wa mabomu Arusha? Fool.
Habari Watanzania wenzangu,

Nimesikitishwa saana na kifo cha ndugu yetu Alphonce Mawazo lakini nasikitishwa zaidi na uvumi unaosambazwa wahusika ni green guard wa CCM nashindwa kuamini moja kwa moja kutokana na maneno yaliopo hapa baada ya uchaguzi katika jimbo alilogombea Alophonce Mawazo.

Baada ya matokeo kutoka wafuasi wa CHADEMA katika jimbo hilo walishangazwa na matokeo yaliotoka kwamba kamanda Alphonce ameshindwa katika uchaguzi huo hali iliozusha sintofahamu kwa wafuasi wa chama hicho kutokana na kushindwa kwake na kutoonekana katika eneo la jimbo tangu siku ya mwisho ya kupiga kura na kutangazwa kwa matokeo.

Kutokana na kutoonekana kwa ndugu Alphonce Mawazo katika jimbo kulileta sintofahamu kwa wafuasi wa CHADEMA ndipo zilipozuka fununu ndugu Alphonce Mawazo aliuza jimbo kwa chama tawala na kukubali kushindwa kirahisi, hali hiyo ilileta chuki kwa makamanda wa CHADEMA hali iliyosababisha waape kwa miungu yote kuwa atakapoonekana hadharani ama zao ama zake lazima wamdhuru, ikibidi hata kumuua.

Hivyo kutokana na hasira za wapenzi wa chama hicho nashindwa kuamini moja kwa moja upande mmoja tuu wa green guard wanahusika kwani kama kushindwa alikuwa ameshashindwa ubunge na hakua tishio tena kwa chama cha mapinduzi, kwangu mimi naweza sema kama angekua tishio kwa chama cha mapinduzi basi wangemdhuru wakati anatafuta jimbo lakini sio kwa sasa ambapo hakuwa mshindani hivyo napata ukakasi sana kuamini kama kuna nguvu yoyoye kutoka chama cha mapinduzi ilio nyuma ya kifo cha kamanda Alphonce Mawazo, lakini pia naona kuna watu wanataka kugeuza kifo cha kamanda Alphonce Mawazo mtaji wa kisiasa.

Naomba tutafakari pia hawa wapenzi wa CHADEMA walikuwa wakiapa kuwa lazima watamdhuru baada ya kuhongwa hela ili akubali kupoteza jimbo lakini pia tukiwa tunasubiri matamko ya police na uchunguzi wao ni vema tukawa watulivu kusubiri uchunguzi wa polisi maana yapo pia mambo nje ya siasa ambayo yanaweza pelekea mtu kuumizwa hata kuuwawa ikiwemo biashara, ugoni, imani za kishirikina, ujambazi. nk

Hivyo kabla hatujanyanyua vidole kunyoosheana kwa hisia na kupandikiza uhasama wa kisiasa ni vema tukatafakari upya na kusubiri vyombo vya dola kuleta ukweli. Nichukue nafasi hii kuwapa pole wafiwa na wapenzi wake MUNGU ALITOA MUNGU AMETWA JINA LA BWANA

Tusivutane sana tusubiri taarifa kutoka polise ndio yenye hatima na ukweli huo.
 
mleta mada nimekuelewa,hilo ni moja,bado mawili muhimu kuhusu tukio hili la ndugu yetu Mawazo
 
Kenge wewe,
Chacha wangwe alikuwa lumumba? Au tunajua mchezo mzima alikuwa shujaa wetu kwetu huku,pongezi kwa kujua mchezo mzima,
Narudi kwa wazo la Uzi huu, utavuna ulichopanda ukiwa duniani,

Wewe ndo kenge...hao waliuwawa kwa kukatwa na mapanga....wewe ni mp.mbavu unaingiza ushabiki kwenye uhai wa watu lofa mkubwa wewe
 
CCM ni nini kitakachowapa hofu muogope kuua wafuasi wa vyama vingine?
Ni kipi cha kikatili zaidi kitakachowaogofya tukitumie?
 
Hata mimi kwa uchungu huku chozi likinilengalenga naunga mkono hoja! Kamanda Mawazo umtuacha katika bahari kubwa ya mawazo!
 
Dah but why? Kuliko kupewa ushindi bora kufuta kabisa
 
Mawazo ni sawa na chacha wangwe na mtikila,
Tena ni sawa kabisa na mtikila. Picha imepigwa Kam vilele ya mtikila, maana picha iko vizuri. Ndiyo maana chadema hapa kukwepa hii lawama ni ngumu
 
Sasa hao ccm kama ndiyo wameua mbona haielezwi ni kwa sababu ipi hadi wamemuua.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom