Msiba wa Mtanzania huyu isiwe ni sababu ya kuongea tuuu bila kipimo au busara....msiba unaumiza ndio, haswa kwa ndugu, jamaa na marafiki wa karibu kwa Marehemu.
Pamoja na kuwa kifo kinatutisha lakini bado ni imani ya tulio wengi kuwa kifo ndio njia pekee ya kwenda kwenye maisha mengine. Bila kujali kifo hicho chanzo chake ni nini anayebaki na ukweli halisi ni Mwenyezi Mungu pekee.
Huu ni wakati wa kusheherekea maisha ya Marehemu Alphonce...na kama mliokuwa karibu naye mnaamini kuwa Marehemu alitamani kuona nchi yenye matumaini, basi tunaobaki tunapaswa kuenzi hayo...na hiyo ndio heshima kwa Marehemu.
Lakini tukiruhusu chuki hasira na kauli za jazba za kulipiza visasi, ni kuwa mnataka tuamini kuwa Marehemu alikuwa muumini wa hayo?
Wengi tulimpenda Kanumba, na wote tunajua kilichosababisha mauti ya mpendwa wetu yule, na tuliacha mamlaka husika zikafanya yale wanayopaswa kufanya na mengine yatabaki ni kazi ya Mola, na tunaamini hivyo ndio maana hatujatoka na kuanza kumpiga mawe Lulu.
Wapo wanaoamini kuwa tasnia ya filamu inaangamia kwa kukosekana Kanumba.....lakini tufanye nini na yameshatokea?
Kifo hakikwepeki na kila mmoja siku moja atakufa, na wapo makumi au mamia au maelfu watakaoumizwa na kifo hicho kutegemea na nafasi aliyokuwa nayo Marehemu.