PreGE2025 Mwenyekiti wa Kampeni ya Mama Asemewe, Geofrey Kiliba, amewataka wanasiasa wanaopinga, kuheshimu jitihada za Rais Samia

PreGE2025 Mwenyekiti wa Kampeni ya Mama Asemewe, Geofrey Kiliba, amewataka wanasiasa wanaopinga, kuheshimu jitihada za Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Wakuu uchawa unakomaa kila siku
==

Mwenyekiti wa Kampeni ya Mama Asemewe, Geofrey Kiliba, amewataka wanasiasa wanaopinga juhudi za Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuacha kupotosha jamii na badala yake kuheshimu juhudi za serikali katika kuleta maendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Machi 15, 2025, jijini Dar es Salaam, Kiliba amesema Tanzania iko salama na hakuna vitisho vinavyohatarisha amani ya nchi. Ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Mama, tukio linalotathmini kazi kubwa ya Rais Samia katika miaka minne ya uongozi wake.

Pia soma Baadhi ya wanachuo wapinga hoja ya Tundu Lissu, ya "No Reform No Election", wasema sio kisemeo cha Taifa

Amesisitiza kuwa Rais Samia amefanya mageuzi makubwa katika sekta mbalimbali, hivyo wananchi wanapaswa kuendelea kumuunga mkono kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Kiliba pia ameainisha kuwa Machi 19, 2025, ni kumbukumbu muhimu kwa taifa, ikitimiza miaka minne tangu Rais Samia aingie madarakani, akiwa Rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania, hatua ambayo ni ya kihistoria na inayopaswa kuenziwa.

 
Hawa wapumbavu huwa mnawaokota wapi?

Na mnawalipa kiasi gani na kutoka fungu gani la fedha?
 
Back
Top Bottom