Frustration
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 3,134
- 4,124
NAMTUMBO -RUVUMA
Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania. Mimi ni mkazi wa mjini Songea ila mzaliwa wa wilaya ya Namtumbo katika kijiji cha Songambele.
Kutoka na maisha ya mjini na changamoto zake nikaamua kuja kijijini kwa ajili ya kilimo cha mahindi ili mambo yaende sawa mjini. Tarehe 10/12/2024 nilihudhuria mkutano wa kijiji na moja ya mambo waliyoazimia ni kwa serikali mpya kwenda kukagua maeneo wanayoishi wafugaji ili kujua wapepokelewa na nani n wanatoka wapi.
Tarehe 27/12/2024 wajumbe 8 walioenda polini wakawa wamekuja na ripoti kamili na baadhi ya majina ya watu waliohusika kuwauzia maeneo wafugaji yalisomwa.
Kwa maelezo ni kuwa ardhi iliyouzwa ni kuwa imeuzwa kinyume na utaratibu,kwani yalitengwa na kijiji kwaajili ya ufugaji nyuki na kilimo cha baadae hivyo yalitengwa.
Katika mkutano huo ilitolewa taarifa kuwa nyumba ya mjumbe mmjo aliyeenda shambani imechomwa moto siku yeye amerudi na alifungiwa mlango kwa nje ni nahati tu mlango wa mbele hauna komeo kwa nje na ndio waliotekea.
Muhanga wa moto alienda kuripoti polisi na katika maelezo yake watu 6 waliotajwa katika ripoti ya uuzwaji wa maeeneo wakawa wahisiwa hivyo wakaitwa polisi.
Polisi kata anamlaumu mwenyekiti wa kijiji ndie chanzo cha kuunguliwa nyumba ya mjumbee wake moto kwa hoja kwamba asingewatuma basi nyumba isingeungua.
Kwa sasa polisi hawazungumzii tena moto bali serikali yote inahitajika polisi kujieleza madaraka ya kwenda kwa wafugaji wameyatoa wapi.
Mitasari imeletwa na wamekili ila wanasema ilitakiwa iende kwanza katani na wilayani ndipo watu wangeenda polini.
Naombeni ushauri wadau wa humu jf ni kweli ni kosa kwa halmashauri ya kijiji kutekeleza agizo la wananchi la kuwahoji wafugaji kwa amani na serikali haikuwa na mamlaka hayo?