Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa aliyepita bila kupingwa akamatwa na Polisi kwa mauaji

Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa aliyepita bila kupingwa akamatwa na Polisi kwa mauaji

Ni ushujaa MwanaCCM akiua mpinzani. Ukihojiwa tamka tu nimeua MwanaCDM utakuwa huru hapo hapo.
 
Subirini muone ngojera za Polisi. Mtaskia hao marehemu walikua majambazi sugu yenye siraha nzito
 
Dah yaani hapa ndio habari imekamilika? Mwenye nyama zaidi juu ya uzi huu tafadhali aziongeze hapa.
 
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Nyakabungo huko Isamilo Mwanza na wenzake wanne wamekamatwa na polisi kwa kuwashambulia na kuwaua vijana watatu wakazi wa Nyakabungo A.

Wakazi wa mtaa huyo wamemlaani mwenyekiti huyo aitwaye Abdukar kwa kuongoza mauaji ya raia wasio na hatia.

Source: ITV habari!
Hao vijana walikuwa vibaka, tukio hilo limefanyika kwenye uwanja wa jeshi, mesi jeshini kando ya barabara ya mawe, nje ya uzio wa kambi ya jeshi.

Ilikuwa saa moja usiku,

Mwenyekiti hakuwepo mwanzo wala mwisho wa tukio.

Kilichofanyika, vibaka walipelekwa kwenye eneo la Uma ili kuepusha kumuingiza raia yeyote kwenye kesi.

Kama polisi wanataka kufaham ukweli, wamtafute jamaa aliyekuwa kavalia shati la njano na alikuwa na filimbi,inaonekana ndiye kiongozi wao(Huyu sio mwenyekiti).

Polisi walionekana kwa mara ya pili, mitaa hiyo jana mchana mida ya saa nane wakifanya forensic. Na Askari mmoja wa kike alionekana kuwahoji baadhi ya wakazi wa eneo lile. Ijapokua usiku wa tukio waliondoka na Binti ' wakamrejesha mida ya saa 10 alfajiri.

Kwa ufupi madogo ni vibaka, kinacho sikitisha watu, vibaka wameuawa wakiwa na umri mdogo wangelipaswa kukanywa tu.

Wazazi tuwe makini na vijana wetu.
 
Ustaarabu ni kitu cha muhimu kuliko mali na vitu vyote hata umilikishwe dhahabu zote nchini mali na vitu vyote kama hujastaarabika vyote ni bure na vita kutesa wewe na kizazi chako
 
msakaa jr,
Unaweza kuthibitisha kuwa ni vibaka?!........maana majirani zako hapo Nyakabungo A wamedai vijana hao siyo vibaka na wamesema Mwenyekiti wa mtaa aliwafunga kamba kisha kwa kushirikiana na wenzake wakawatoa uhai!

Katika hili itikadi nimeweka pembeni!
 
Unaweza kuthibitisha kuwa ni vibaka?!........maana majirani zako hapo Nyakabungo A wamedai vijana hao siyo vibaka na wamesema Mwenyekiti wa mtaa aliwafunga kamba kisha kwa kushirikiana na wenzake wakawatoa uhai!

Katika hili itikadi nimeweka pembeni!
Siishi Nyakabungo,

Mwenyekiti alikuepo eneo la tukio? Alikutwa eneo la tukio? Mwenyekiti alikamatwa akiwa wapi? Unadhani kama umehoji ndugu wa wahanga /wenye chuki na mwenyekiti watasema hao ni vibaka?

Je umewahi kusikia kisa chochote cha dokta kuvunjwa mguu na vibaraka maeneo hayo( Nyakabungo)? Au tukio la ubakaji la Binti akiwa na mama yake?? La ulawiti je alilofanyiwa mtoto WA mwenyekiti aliye maliza muda wake?

Katika tukio lolote huwa hapakosekani makundi mawili. Kwasababu umeamua kuliamini kundi moja, mimi Sina msaada wowote katika hilo.
 
Una uhakika? Wale makada wa ccm waliomuua Godfrey Luena wamefanywaje?
Mkuu kuhukumiwa kunategemea na mahakama kujiridhisha pasipo shaka kuwa wahusika wametenda au laa,ingekuwa ni kuhukumu tu huenda wote tungekuwa gerezani.
R.I.P G.Luena diwani kata ya Nawawala.
 
Mlipo muua alfonce mawazo rip mlichukuliwa hatua gani kama hamhalalishi mauwaji?
Mkuu sio jambo jema kuhusisha watu/chama moja kwa moja kwa sababu mauaji hutokea sio kwa sababu tu ya siasa laa,Kuna Mambo mengi ya kijamii pia.
R.I.P A.Mawazo.
 
Ni fitna tu za kisiasa, huyo atakuwa ni wa upinzani - chama chetu kina watu safi...mtu aliyechaguliwa na wananchi wote bila kupingwa hawezi kufanya ushenzi huo - haiwezekani.

CCM - JUUU....!!
CCM - SAFIII.....!!
 
Mkuu sio jambo jema kuhusisha watu/chama moja kwa moja kwa sababu mauaji hutokea sio kwa sababu tu ya siasa laa,Kuna Mambo mengi ya kijamii pia.
R.I.P A.Mawazo.
Mtakapohusishwa na Mungu wakati anadai damu ya mawazo mikononi mwenu utaelewa zaidi.kwa sasa weka siasa tu za kutetea hata dhambi.Mfano mdogo tu kwako VIONGOZI wa chadema wapo mahakamani kwa kifo cha Aquilina rip japo aliyeuwa yupo anadunda.Mungu atamlenga aliyeuwa si kina mbowe kama mfanyavyo nyinyi.
 
Back
Top Bottom