PostGE2025 Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha Bodaboda: Serikali iwachukulie hatua wanaoharibu amani

PostGE2025 Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha Bodaboda: Serikali iwachukulie hatua wanaoharibu amani

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha Bodaboda wa Tawi la CBT wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Amiri Ali, ameitaka Serikali kuwachukulia hatua za kisheria watu wote wanaohamasisha na kushiriki vitendo vya uvunjifu wa amani kama sehemu ya kuimarisha amani na utulivu nchini.

Ali ameeleza hayo leo Desemba 09, 2025 katika mahojiano maalumu, kuhusu hali ya amani wilayani Kahama ambapo amesisitiza kuwa vijana wengi ni tegemeo katika familia zao na inapotokea vurugu na uvunjifu wa amani wamekuwa wakiathirika kiuchumi kutokana na kushindwa kufanya kazi zao.

Ametoa wito pia kwa madereva wenzake wa bodaboda kujitenga na matukio ya uvunjifu wa amani yanayohamasishwa kupitia mitandao ya kijamii, akieleza kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii hivyo kila mmoja anawajibika katika kuilinda.

 
Back
Top Bottom