Mwenyekiti wa UVCCM, Kigoma: Abuya awataka Vijana kuwajibika na kuonyesha Uadilifu katika Uongozi

Mwenyekiti wa UVCCM, Kigoma: Abuya awataka Vijana kuwajibika na kuonyesha Uadilifu katika Uongozi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kigoma, Ndugu Emanuel Abuya, amekutana na wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa vijana, akisisitiza umuhimu wa uwajibikaji katika nafasi zao za uongozi. Alisema kuwa chama kina imani kubwa na vijana, hivyo ni jukumu lao kuonyesha mfano bora kwa vitendo. "Twende tukathibitishe kuwa vijana tunaweza kuongoza kwa uadilifu na tija," alieleza.
IMG_1392.jpeg

Aidha, Ndugu Abuya alibainisha kuwa uwajibikaji wa vijana utafungua njia kwa wengine kupata nafasi zaidi za uongozi.

Ndugu Abuya Alitoa rai kwa vijana kuonyesha nidhamu na kujituma, akisema kuwa maadili bora ni msingi wa maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla. Kikao hicho kimeacha ujumbe mzito wa kuimarisha nafasi ya vijana katika maendeleo ya nchi.
IMG_1393.jpeg
 
Back
Top Bottom