Haya yote yametokana na mfano anaounesha mwenyekiti wa chama na rais wa nchi, kama akina james wanatoa kauli za kuchochea mauaji na chama chake kinakaa kimya basi ni wazi kuwa wanabariki ujinga huo.
Nimemkumbuka dikteta Life President of Malawi, Hastings Kamuzu Banda 'Ngwazi' na kikundi chake cha vijana ndani ya chama tawala cha MCP, walikua na nguvu kuliko vyombo vya usalama vya nchi, walitesa na kuua wapinzani. Mwisho wa siku jeshi la malawi ndilo lililazimika kukisambaratisha kikundi hiki baada ya Ngwazi kuangushwa.
TPDF, TPF na TISS mnao wajibu wa kuilinda nchi hii dhidi ya matishio ya ndani na nje, UVCCM na kikundi hatari kwa usalama wa nchi hii, mkiendelea kukilea tutakuja kuchinjana kwama Rwanda.