Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa ahamasisha Mbowe, Zitto na wengine wanaoikwamisha Serikali 'washughulikiwe'

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa ahamasisha Mbowe, Zitto na wengine wanaoikwamisha Serikali 'washughulikiwe'

Mwenyekiti wa Uvccm Taifa Heri James amewalaumu vijana wa CCM Tanzania kuwaacha wanasiasa wa upinzani Zitto Kabwe na Freeman Mbowe wakitembea mitaani bila kubughudhiwa/kushambuliwa kwa madai kuwa wanataka kulipasua taifa kwa vitendo vyao vya kuhujumu Serikali na Taifa

Naye Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa, Kenani Kihongosi amesema wapinzani wanaoichafua Serikali wanapaswa kukosolewa au Kuuawa kabisa.

Cc: Shige2
 
Hivi uchochezi maana yake nini?Kuna mjinga mmoja alisikika akisema sheria awamu hii sio msumeno!
 
Vijana stupid, na kauli hizi hazitoki midomoni kwa bahati mbaya, Huyo Heri James alikuwa akisoma kwenye karatasi. Yaani ccm na ukubwa wake inaongozwa na vijana wajinga kabisa ambao hawana uwezo wa kujua baya au zuri la kuongea mbele ya hadhara?!
 
Enzi ya Hayati baba wa taifa Mwl Julius Nyerere

Hawa vijana wasingepewa japo nafasi ya ujumbe nyumba kumi.

Wangekuwa ndani na kuhojiwa kama sio kupigwa marufuku kwenye uongozi wa aina yoyote.

Wange pelekwa vijijini nakufungiwa huko wakiripoti kila siku kwa mtendaji wa kijiji kwa maisha yao wote.

Hawa niwanyama- sio binadamu

Wanahubiri Mauji, kutesa nakuteka watanzania!!!!! Hadharani.
 
Siku hizi sheria ni shoka, unakata unainua
Siku hizi sheria ni chaini za kupigana kwenye Kung fuu
Kadri unavyoizungusha inakugonga mwenyewe kabla hujamfikia adui
 
Hii nchi imefikia hatua ya kutisha ya kuogofya. Siku hizi matamko yanatolewa hadharani ya kuuwa?. Halafu wanaangaliwa tu wahubiri utumbo?. Tumefika mbali sana,tumerudi nyuma enzi za ukoloni. Hawa wanaotoa haya matamko wasipodhibitiwa wataiachia hii nchi maumivu makubwa. Pamoja na kwamba wana dola lakini hawana uwezo wa kuwadhibiti umma yakiibuka machafuko ya wenyewe kwa wenyewe. Wanafikiri wanasaidia kumbe ndio wanachochea petrol kwenye jumuiya ya kimataifa. Halafu bahati mbaya ndio vijana wanaoitwa wasomi. Hii ni hatari kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenyekiti wa Uvccm Taifa Heri James amewalaumu vijana wa CCM Tanzania kuwaacha wanasiasa wa upinzani Zitto Kabwe na Freeman Mbowe wakitembea mitaani bila kubughudhiwa/kushambuliwa kwa madai kuwa wanataka kulipasua taifa kwa vitendo vyao vya kuhujumu Serikali na Taifa

Naye Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa, Kenani Kihongosi amesema wapinzani wanaoichafua Serikali wanapaswa kukosolewa au Kuuawa kabisa.
Chama chochote kinapoelekea kufa huja na hoja kama hizi .
 
Mwenyekiti wa Uvccm Taifa Heri James amewalaumu vijana wa CCM Tanzania kuwaacha wanasiasa wa upinzani Zitto Kabwe na Freeman Mbowe wakitembea mitaani bila kubughudhiwa/kushambuliwa kwa madai kuwa wanataka kulipasua taifa kwa vitendo vyao vya kuhujumu Serikali na Taifa

Naye Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa, Kenani Kihongosi amesema wapinzani wanaoichafua Serikali wanapaswa kukosolewa au Kuuawa kabisa.
Pompeo anazidi kukusanya ushahidi tu. Mungu mbariki Pompeo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama vp walianzishe basi tuone nani ataibuka mshindi. Hao uvccm kwanini wanaongea tu waanzishe mapambano.
Hao UV ccm wawaambie wafuasi wao huku mtaani wawashambulie vijana waliopo upinzani nadhani si zaidi ya wiki watu wote huku kitaa watakuwa upinzani
 
Hii nchi imefikia hatua ya kutisha ya kuogofya. Siku hizi matamko yanatolewa hadharani ya kuuwa?. Halafu wanaangaliwa tu wahubiri utumbo?. Tumefika mbali sana,tumerudi nyuma enzi za ukoloni. Hawa wanaotoa haya matamko wasipodhibitiwa wataiachia hii nchi maumivu makubwa. Pamoja na kwamba wana dola lakini hawana uwezo wa kuwadhibiti umma yakiibuka machafuko ya wenyewe kwa wenyewe. Wanafikiri wanasaidia kumbe ndio wanachochea petrol kwenye jumuiya ya kimataifa. Halafu bahati mbaya ndio vijana wanaoitwa wasomi. Hii ni hatari kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanasoma lakini hawapewi maarifa, unajiuliza ina maana hata elimu ya uraia hawakupata? sasa wako vyuoni hiyo development studies hawajasoma kwamba huwa kuna conflict of ideas? ni mambo ya kushangaza kweli. Ndo maana waajiri wengi wanalalmikia quality ya wanaomaliza vyuo. Kwenye makaratasi wamefaulu kwenye practical zero.
 
Uvccm kama vipi lianzisheni tuu hakuna noma kabisa, uweni tuuuuuu, hakuna shida.
Tunataka tuone outcome ya matamko yenu.
 
Tarehe 10/2/2019 Ngome ya Vijana tulitoa ujumbe kupitia kwenu uliosema ''UVCCM WAMEAMUA KUWA INTERAHAMWE POLISI IWADHIBITI KABLA SISI HATUJAWADHIBITI''.

Juzi zimesikika kauli za Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Kheri James na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa Ndugu Kennani Kihongozi kuwa Kiongozi wa Chama chetu Ndugu Zitto Kabwe auliwe.

Kauli hii ya UVCCM ilitanguliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuruhusu mjadala usiokuwa na maana na uliojadili waziwazi kumuua Zitto Kabwe bila Spika Job Ndugai kudhibiti hoja hizo za kijinga na zinazodhalilisha Bunge letu tukufu.

Sisi tunajua uvccm ilishakufa zamani waliobaki ni wachumia tumbo ambao wanaongea bila kuangalia athari ya maneno yao kwa mustakabali wa ulinzi, usalama na Amani ya Taifa letu ili waendelee kubebwa kwenye ulaji usiozinagita maslahi ya Taifa letu.
Pamoja na hayo ngome ya vijana tunawataka uvccm waanze, Sisi tutamaliza kwa vitendo kwamaana tumechoka maneno.

Spika wa Bunge ndugu Job Ndugai anajua Tanzania imeingia mikataba ya kimataifa na ile ya kikanda na anajua ukishaingia kwenye mikataba hiyo lazima utii na kuheshimu mikataba hiyo.

CCM inajua ukweli kuwa anayezuia pesa za mkopo wa elimu unaotolewa na Bank ya dunia siyo Zitto Kabwe bali Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi, Rais John Pombe Magufuli baada ya kauli yake ya kibaguzi ya kuzuia watoto waliopata ujauzito kutokuendelea na shule baada ya kujifungua kinyume na mikataba ya kimataifa tuliyoingia, kimyume na sera za vyama vyote hapa nchini ikiwamo CCM yenyewe.

Ngome ya vijana inaamini siku Rais John Pombe Magufuli ataifuta kauli yake ile na kuruhusu watoto wanaopata ujauzito kuendelea na masomo baada ya kujifungua Benki ya Dunia itatoa mkopo huo mapema sana.

Ngome ya Vijana tunapinga na kulaani kauli ya Spika Ndugai kuwa Zitto Kabwe alivoiandikia Benki ya Dunia barua alifanya jinai na hivo achunguzwe, tulitegemea Zitto Kabwe apongezwe na Bunge kwa kitendo chake cha kishujaa.

MSIMAMO WETU.

1. Ngome ya vijana tumejiandaa vya kutosha kumlinda na kumuhami Kiongozi wetu dhidi ya uovu wowote. Dalili zozote za uchokozi dhidi ya Kiongozi wetu tutazijibu kwa vitendo.

2. Tunavitaka vyombo vyetu vya ulinzi na usalama visifumbie macho kauli za kumwaga damu zinazotolewa na viongozi wa CCM. Ukimya wa vyombo vya ulinzi na usalama unaonesha waziwazi kuwa wanakibeba Chama cha Mapinduzi.

3. Tunamtaka Msajili wa Vyama vya Siasa kuichukulia hatua CCM kwa kauli hizi za mauaji zinazotolewa na Viongozi na wabunge wa CCM ambazo kwa hakika zinakwenda kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa.
 
CCM ombeni radhi vinginevyo lolote lukimkuta zito hata tu na wafitini mjue itakula kwenu mtachomewa nyumba watoto na viongozi wa ccm ngazi za mitaa watatekwa na kuchinjwa huku wakirekodiwa mauwaji jamaa ya isis msikubali kauli za wabunge wenu wapumbavu jitengeni nazo mkisafishe chama chenu CCM mnamaadui wengi hamjui Nani atatembekea kauli zenu na kuwafitini
 
Back
Top Bottom