Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameamua kujiuzulu nafasi yake

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameamua kujiuzulu nafasi yake

Hili linyonyaji linalojiita mulinzi ndo linaharibu soka hapa nchini. Wizi, rushwa, upangaji wa matokeo, ufisadi na matakataka mengine yote kwake ni marashi. Hovyo kabisa hili dudumizi.
Kabla ya manji yanga ilikuwa na migogoro ya yanga Asili na kampuni, yanga imenyonywa nini? Yanga haikuwa na Amani sasa inatejea kulekule kwenye shida.
 
View attachment 382142
Habari za uhakika ambazo tumezipata kutoka katika chanzo cha uhakika ndani ya Yanga zinaonyesha kuwa mwenyekiti wa Yanga Bw Yusuf manji ameamua kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa yanga pamoja na kusitisha kusudio lake la kuichukua na kuendesha kibiashara timu ya Yanga na nembo yake .

Hili ni anguko kuu kwa yanga endapo Bw Yusuf manji atajionda Yanga kutokana na ukweli kuwa tayari mahasimu wao wa jadi Simba wanakamilisha taratibu za kumkabidhi timu Bw mohamed Dewji MO.

Uamuzi wa manji kujiondoa yanga unatajwa kuchangiwa na shutuma zinazotolewa na baadhi ya viongozi wa serikali, na wengine kutoka ndani ya yanga ambao wanatumiwa na baadhi ya wafanyabiashara kwa maslahi yao binafsi na sio ya yanga.

Manji anaonekana kuchoshwa na tabia za baadhi ya watu kumtukana na kumkebehi kwa hatua yake ya kuichukua timu ya Yanga na sasa ameamua kukaa pembeni kulinda heshima yake .

Hata hivyo viongozi wa Secretary ya yanga siku nzima ya leo wameonekana kuchanganyikiwa uku baadhi wakiwa wanapigana vikumbo kuingia na kutoka quality plaza zilizopo ofisi za Bw manji hatua inayoashiri kuna jambo kubwa linatokea.


Chanzo: Shaffih Dauda
mpango wa manji hauna uwazi wala tija kibiashata kwa wanachama wa yanga. huwezi kukodi yanga kama taxi bubu. kama kweli manji anataka kuisaidia yanga na sio kuikamua angesaidia kufadhili mpango wa kuigeuza yanga kua kampuni kwa uwazi kwa kupata thamani halisi ya yanga kabla ya yeye kusema apewe kununua hisa ngapi. sio mtu unaweka hela yoyote mezani eti anakodisha yanga. waswahili kuona hela karibu wampe manji yanga bure.
 
Kabla ya manji yanga ilikuwa na migogoro ya yanga Asili na kampuni, yanga imenyonywa nini? Yanga haikuwa na Amani sasa inatejea kulekule kwenye shida.
Mkuu sizungumzii yanga tu, angalia sasa hivi karibu vilabu vingi vinavurugwa na hili dudumizi. Mifano michache ni stand united, yanga, nk. Utasema hili takataka halihusiki kuharibu soka? Karibu.
 
Anawadai shilingi ngapi?
Yale majengo lazima wampe afidie deni lake.
 
Kuna wajanja wamebuni mbinu za kula pesa wakaenda kwa Manji kumdanganya kuwa Mengi anataka Timu na manji amepagawa kuna ujanja unafanywa na madalali wa soka la maji taka.
manji akisikia jina la godfather mengi, tumbo la kuhara linampata mda huo huo.
 
Whatever the case, Yanga itasonga mbele. Kama ni kweli yule mtu wa 65 billion ajitojeze mapema.
Bado mnaendelea na akili za kumtegemea mtu mmoja mmoja? Na huyo wa bilioni 65 akijitoa ghafla katikati ya msimu, mtaanza kutafuta mwingine? Kwa hizi timu za wanachama, ni lazima wanachama wawe sehemu kubwa ya kuridhisha ya uendeshaji wa timu
 
Walivyo wazembe watakwenda kumpigia magoti....

Kama walivyofanya wakati ule aliposema hagombei tena ...


magoti.jpg
 
Hii nchi ni majungu matupu ndio maana hatupigi hatua.
Magufu wanyooshe watanzania angalau miaka 5 kumaliza hizi blabla na kula kwa fitna
 
image-jpeg.349922


Wanachama na mashabiki wa Yanga wakiyachana na kuyachoma moto magazeti ya The Guardian na Nipashe yanayomilikiwa na kampuni ya IPP MEDIA ambayo ipo chini ya Reginald Mengi.
 
Hii nchi ni majungu matupu ndio maana hatupigi hatua.
Magufu wanyooshe watanzania angalau miaka 5 kumaliza hizi blabla na kula kwa fitna
Umesema kweli mkuu!! Hii nchi imejaa majungu, fitna na ushabiki wa kijingajinga tu! Na hii inaenda hadi kwenye mambo serious ya maendeleo ya nchi! Kila kitu kujifanya wajuaji!
 
Na mm Yanga, basi... sintachangia hata shilingi...!!

Manji kajitoa sana kuibeba Yanga kwa miaka... Uongozi wa Yanga kazi majungu tu na uchawi...!!
Ole wao nisikie sijui wanataka michango... ndio wakome
 
Nimeumia sana sanaaa Manji kujiuzulu... sana..na Yanga mtakufa kibudu... nahasira, na mmeniudhi...!! nahama Yanga.. huu sasa ni ubwege kupitiliza.. Manji ameisadia kwa hali na mali Yanga.. kutoka moyoni mwake... ametubeba kwa kila msaada.. alafu uongozi wa Yanga umeacha ujinga na majungu yaendelee, wakati wote huo Yanga inafanya vizuri hao watu wa majungu, uchawi na wapuuzi walikuwa wapi..?

I feel very disappointed... nimeumia sana... Sitaki tena nisikie sijui nn wala nn.. Yanga mtajiju..!! Machizi nn Uongozi wa Yanga... toka kuleee... mkafie mbali....
 
Back
Top Bottom